Habari za Punde

Sera ya menejimenti ya Utumishi wa Umma kufanyiwa mapitio

Na Raya Hamad OR-KSUUUB
  
Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora imedhamiria kuifanyia mapitio na    kuimarisha sera ya menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mikakati yake ambayo ni moja ya nyenzo muhimu katika usimamizi wa utoaji huduma nchini.
 
Naibu Katibu Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndugu Seif Shaaban Mwinyi anaeshughulikia masuala ya utumishi ameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mwelekeo wa sera ya usimamizi wa  Utumishi wa Umma  na utekelezaji wake katika kuimarisha Utumishi wa Umma Zanzibar

Ndugu Seif amesema Sera ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma inawagusa wananchi wote wa Zanzibar hivyo ikiwekewa mkakati sahihi mafanikio yake yataweka misingi imara ya usimamizi wa huduma utowaji huduma na upatikanaji wa huduma bora za umma kwa kadiri siku zinavyokwenda .

Aidha amesema Sera tokea ilipotungwa mwaka  2010 yapo mambo mengi yaliyofanyiwa kazi katika utekelezaji na mafanikio makubwa yalipatikana ikiwemo  Uundwaji wa Taasisi  na vyombo mbalimbali vya usimamizi wa udhibiti katika utumishi wa umma, utungaji wa sheria na miongozo kusimamia na kudhibiti utumishi wa umma, marekebisho katika mifumo ya malipo ya mishahara pamoja na mafao baada ya kustaafu 

Mifumo ya upangaji na uendeshaji watumishi , Ujenzi wa Ofisi za Kisasa, matumizi ya mifumo ya ki elektronik katika shughuli za utumishi wa umma ikiwemo kufungwa kwa kuwekwa mifumo ya habari na mawasiliano wizarani , ugatuzi wa majukumu kwa mamlaka za serikali za mitaa ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa jamii

Hata hivyo pamoja na juhudi zilizochukuliwa katika utekelezaji wa Sera bado kumekuwepo na changamoto kadhaa katika upatikanaji wa huduma za umma hapa nchini yakiwemo ongezeko la idadi ya watu jambo ambalo hulazimisha ongezeko la mahitaji ya huduma za umma, ongezeko la shughuli za kiuchumi na kukua kwa uchumi, kukua kwa ushindani katika Nyanja mbali mbali za uzalishaji 
Kukua kwa matumizi ya teknolojia, miundombinu mbalimbali katika mahitaji ya kijamii na kiuchumi ni miongoni mwa mambo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi  kwa mikakati maalumu ambayo italeta mabadiliko yatakayoiwezesha Serikali kukabiliana na changamoto hizo .

Kiongozi na mkurugenzi  wa mradi wa kusaidia watendaji wasio wa kitaifa wa Zanzibar   Fergan Ryan  amesema malengo na matarajio ya kikao hicho ni kutafakari kwa pamoja juu ya mpango wa utekelezaji wa  mpango wa kuimarisha Utumishi wa Umma Zanzibar na kuelezea hali halisi ilivyo kwa sasa changamoto na hatimae kupokea maoni na michango itakayosaidia kuzingatiwa katika uandaaji wa program ya pili mabadiliko ya Utumishi wa Umma 
 

Nae Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti wa Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi Daima Mohamed Mkalimoto  amesema Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini  Zanzibar umeweka msisitizo wa kupatikana kiwango cha juu cha utawala bora na kuondokana na  umasikini pamoja na kutambua umuhimu wa nafasi ya usimamizi wa Utumishi wa Umma katika kuyafikia malengo ya maendeleo ya Zanzibar.

Bi Daima amesisitiza washiriki hao na  kuwakumbusha kuwa wote ni watumishi wa Umma na wanajukumu la kufanya kazi kwa kufuata Sera inayowaongoza  hivyo kufanyakazi kwa uhakika kutaleta mageuzi  kwa vile Sera inatamka kuwa “Dhima ya Utumishi wa Umma Zanzibar ni kutoa huduma bora kwa ufanisi na tija kwa umma wa Zanzibar na kwa kiwango cha juu cha uadilifu na heshima”

Aidha amewakumbusha washiriki hao kuwa Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni msimamizi lakini Idara na Taasisi zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanalo jukumu la kuwahudumia wananchi na wajibu  wa kutekeleza kwa vitendo badala kufanya kazi kwa mazoea.

Nao washiriki wa mkutano huo wamesema kuwa ni muhimu kufanyiwa mapitio kwa sera zilizopita  kabla ya kuanza na sera mpya, masuala ya Utumishi wa Umma lazima taasisi ziungane pamoja na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi pia sheria zifanyiwe mapitio ili ziweze kufanyiwa kazi 

Pia wamesisitiza suala la kuwekwa kwa kumbukumbu sahihi za watendaji na watumishi wa umma kwani wakati wakustaafu hutokea changamoto nyingi ikiwemo kujitokeza utofauti ya tarehe ya kuzaliwa kwa mhusika mmoja ambae huonekana katika vitambulisho vya ZSSF, Cheti cha kuzaliwa, leseni ya udereva , kitambulisho cha Mzanzibari , kitambulisho cha Benki nk jambo ambalo linapelekea usumbufu kwa jamii na watendaji 

Mada zilizojadiliwa ni pamoja masuala ya usimamizi na uwajibikaji , tathmini, uwekaji wa kumbukumbu viinuwa mgongo, pencheni, usimamizi wa rasilimali watu,  usimamizi wa kumbukumbu na taarifa , serikali za mitaa  

Mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha maafisa  watumishi na maafisa mipango kutoka Taasisi tofauti za SMZ na baadhi ya watendaji tofauti umeandaliwa na  Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora  unafadhiliwa kwa pamoja kati ya EU  na  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kushirikiana  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.