Habari za Punde

siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu duniani yaadhimishwa Zanzibar

Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar.                           

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaweka mipango madhubuti ya kisera,Kisheria na program mbali mbali ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashirikishwa katika masuala mbali mbali ya maendeleo.

Hayo aliyasema katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu duniani yaliyofanyika huko Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil alisema sio jambo jema kwa mtu yoyote katika jamii kuwatenga watu wenye ulemavu kwani sote ni walemavu watarajiwa.

Aidha alisema kuwa haipendezi kwa watu hao kunyanyaswa  , kuwanyanyapaa  na kuwatendea matendo yaliyo kinyume na haki za binaadamu katika maisha yao , tuelewe watu hao wanahitaji kuthaminiwa , kutunzwa na kuenziwa utu wao kama ilivyoainishwa katika katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na sheria ya watu wenye ulemavu.

“Tuache tabia ya kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu kwani tukumbuke na sisi ni walemavu watarajiwa , pia na wao hawakutaka kuumbwa na ulemavu ila rehema zake allah”. Alisema Balozi Seif.

Pia kwa kitaalamu huwezi kuwaongoza watu wa aina yeyote ile bila ya kuwajua watu wanaoongozwa wakoje na mahitaji yaqo ni yepi m hivyo kwa kujua suala hilo , Idara ya watu wenye ulemavu inaendelea kufanya usajili wa watu wenye ulemavu kwa kuanzisha mfumo wa takwimu unaojulikana kwa jina la “Jumuishi Database”ambayo imezinduliwa leo mradi ambao umeungwa mkono na Taasisi inayoshughulikia masuala ya Idadi ya Watu duniani.

Balozi Seif amewaonya akinamama wanao tabia ya kuwafungia watoto wenye ulemavu ndani bila ya kuwashirikisha kwenye elimu na akinamama wenye tabia ya kuwadhuru watoto wao kwa makusuudi na kuwatia ulemavu.

“Ole wao kwa wale akinamama wanaowafungia ndani watoto wenye ulemavu  na wale wanaowatia watoto wao adabu na kuwatia ulemavu kama vile kuwamwagia maji moto”. Alitoa onyo Balozi Seif.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud  amesema  iwapo database itakapokamilika itaweza kutusaidia kujua idadi kamili ya watu wenye ulemavu  , pia hata majengo yanayojengwa yanazingatia watu wenye ulemavu.

Pia alisema kuhusu omba omba waliyoenea katika Mkoa huo iwapo kutakuwa na mashirikiano kuna uwezo mkubwa wa kuwaondosha na tutashirikiyana na Makamo wa pili kuhakikisha watu hao hawapo tena .

Sambamba na hayo msoma risala kutoka shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Zeyana Ahmad   amesema  tunaomba kuanzishwa utaratibu wa kutumia lugha za alama  sehemu za hospital , mahakamani, polisi na sehemu zenye mkusanyiko wa jamii.

Pia wameiomba serikali iwaajiri walimu maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu na kuwekwa bima ya afya  kwa watu hao.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika siku ya walemavu ambayo inaadhimishwa dunia nzima “KUWAWEZESHA WATUN WENYE ULEMAVU NA KUHAKIKISHA UJUMUISHWAJINA USAWA. Kauli mbiu hii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.