Habari za Punde

UKARABATI WA MIUNDO MBINU YA BARABARA JIMBO LA VUNJO KUREJEA JANUARY

Mwenyekiti wa Tahsisi ya Maendeleo ya Vunjo (VDF) Askofu Mstaafu wa KKKT dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin sham akizungumza wakati wa Sherehe ya siku ya Wanavunjo (Vunjo Day) iliyofanyika chuo cha Ualimu Marangu na kukutanisha wananchi na viongozi mbalimbali.
Mbunge wa jimbo la Munjo na Katibu wa Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo (VDF) Mh James Mbatia akizungumza katika sherehe hizo ambas zinafanyika kwa mara ya kwanza Latina jimbo hilo na kukutanisha wenyeji wa Vunjo waishio nje na ndani ya jimbo hilo.
Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kijitonyama ,Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Eliona Kimaro ambaye pia ni mwenyeji wa Jimbo la Vunjo akizungumza latina sherehe hizo.
Viongozi mbalimbali walioshiriki katika sherehe hizo wakipiga makofi .

VUNJO-KILIMANJARO 
MBUNGE wa Vunjo, James Mbatia amesema kuanzia wiki ya pili ya mwezi Januari mwaka ujao, mitambo yote ya ujenzi wa barabara iliyokuwa imezuiwa na serikali ya Wilaya ya Moshi kuendelea na kazi za upanuzi wa barabara, itarejea kazini.
Alitangaza uamuzi huo mbele ya mamia ya wananchi, viongozi wa dini mbalimbali, madiwani na watendaji wa vjijiji waliohudhuria hafla ya siku ya wana Vunjo iliyofanyika Chuo cha Ualimu Marangu, Wilaya ya Moshi.
“Tumeingiliwa lakini tujipe moyo kwa sababu jambo lolote likipata msukosuko sana, ni jambo lenye heri. Mwezi wa 11 mwaka huu Rais (Magufuli) aliagiza kazi hii iendelee mara moja, kwa hiyo naomba nitangaze kwa niaba ya bodi ya VDF (Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo), wiki ya pili ya mwezi Januari 2019, vyombo vyote vinarudi kazi na kazi inaendelea,”alisema Mbatia
Wakati Mbatia anatangaza uamuzi huo, tayari upanuzi na ujenzi wa barabara hizo za vijijini katika Jimbo la Vunjo kwa kiwango cha changarawe, umezuiwa na serikali Wilaya ya Moshi.
Mradi huo unahusisha barabara zenye urefu wa kilometa 389.3 ambazo zitagharimu sh. bilioni 12.077 kutokana na utafiti wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura).
Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kijitonyama wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Eliona Kimaro alisema maendeleo ya mtu na utu wake na nguvu ya jamii ndivyo pekee vinavyoweza kuchochea kuleta maendeleo katika nchi yeyote ile.
“Nguvu ya jamii katika kuleta maendeleo na kutatua matatizo yao binafsi na ya serikali ni kinyume kabisa katika maendeleo kwa kanuni za kiuchumi.
Zaidi Much, Kimaro alieleza: "Kufikiri kwamba nchi tu ndiyo inaweza ikaleta maendeleo ni makosa, ndio maana wanasiasa wengi wa Marekani wamekuwa wakisema ili uwe Rais wa nchi au kiongozi wa serikali lazima uwe na mawazo haya, kwamba unakwenda kuifanyia nini nchi na sio nchi imfanyie yeye,”alisisitiza 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa VDF ambaye ni Askofu Mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao alisema dhamira ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni si kuboresha tu miundo mbinu ya barabara, bali pia kuna sekta za afya, elimu, maji na sekta ya mazingira.
Alisema taasisi hiyo ndio mwanga wa alfajiri uliopewa jina la ‘ngatuni yetu’ ambayo inataka kuifanya Tanzania kuwa sehemu bora, salama na pazuri pa kuishi, kwa vile itatekeleza jukumu hilo nchi nzima.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.