Habari za Punde

Wananchi Wajitokeza Hospital Kuu ya Mnazi Mmoja Kufanyiwa Uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi.

Mratibu wa Mradi wa Uchukuzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi Zanzibar Dkt. Omar Mwalim Omar  akimkaribisha Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma  katika Tiba ya Uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya  Kizazi inayofanyika Hospitali  ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Mratibu wa Mradi wa Uchukuzi wa Saratani ya Singo ya Kizazi Zanzibar  Omar Mwalim Omar akimuonyesha jambo Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma  wakati alipowatembelea Madaktari wanaoendelea kutoa matibabu Hospitalini hapo.
Naibu Spika  Mhe. Mgeni Hassan Juma akipata maelezo  kutoka kwa  Daktari wa Maabara Kibwana Omar Kibwana wakati alipotembelea Chumba hicho cha Maabara Hospitalini hapo (kulia)  Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman.
Mtaalamu wa Magonjwa ya Saratani ya Shingo ya Kizazi Hospitali ya Mnazi mmoja  Dkt. Abdalla Yusssuf Mohamed  akimpatia maelezo  Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma  wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma akizungumza na Wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya Uchukuzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi  (kulia)  Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman.

Baadhi ya Vifaa vinavyotumika kwa ajili ya kufanyia  Uchukuzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi Hospitalini hapo. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.

Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.
Jumla ya kinamama 1,339 wamejitokeza katika uchunguzi pamoja na kufanyiwa vipimo vya maradhi ya kensa ya shingo ya kizazi katika hospitali kuu ya mmanazi mmoja mjini Unguja.
Mratibu wa mradi wa uchunguzi wa kensa ya shingo ya kizazi,Dk. Omar Mwalimu Omar alitoa kakwim hiyo huko hospitali ya mnazi mmoja wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara maalum ya kutembelea eneo linalo endeshwa zoezi hilo.

Amesema katika zoezi hilo lililoanza Jumatatu iliopita hadi leo (Jumatatu) watu 36 kati hao wametiliwa mashaka na kufikia maamuzi ya kuchukuliwa vinyama ili kuchunguzwa kwa hatua nyengine na baadaye yatatoka majibu rasm ya afya zao.

“Mara baada ya kuwafanyia uchunguzi mwengine na pindi tukibaini kuna mwenye maradhi hayo , tutaanza naye kwa kumpata tiba kwa kutumia dawa kwa mujibu wa taratibu za kitaalam”alisema Dk Omar.

Naye mtaalamu wa magonjwa ya saratani katika hospitali ya mnazi maoja, Dk Abdalla Yussuf Mohamed alisema katika zoezi hilo wanachunguza vinasaba vyote vya akinamama hao ambavyo ni muhimu katika uchunguzi huo.

Mapema Naibu Spika Mgeni Hassan Juma alisema ni vyema wakaongezwa wataalamu wazalendo katika kupata kujifunza kutoka kwa watalamu wakichina waliopo.

Aidha aliwapongeza akinamama hao waliojitokeza katika zoezi hilo na kuwataka waendelee kuwahamasisha wenzao ili zoezi hilo lifanikiwe kama lilivyokusudiwa.

Hatahivyo aliomba wizara ya afya kuangalia uwezekano wa uchubguzi kama huo kupelekwa Pemba na haospitali za mikoa ili idadi ya uchunguzi wa akinamama uongezeke.

Kwa upande wa Naibu waziri wa Afya, Harusi Suleiman alisema lengo la serikali ya mapinduzi Zanzibar ni kuona kinamama wanapewa matibabu bora ili kutatua changamoto za maradhi yanayowasibu.

Mradi huo wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi unaendeshwa na serikali ya china kwa muda wa miaka minne, ikiwa ni jitihada za Rais  wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.

1 comment:

  1. ahsante kwa taarifa ya hospitali, lakini taarifa hii imechanganya majina ya watu na picha zao pamoja na kazi zao.....

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.