Habari za Punde

Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu Awahamasisha Wabunge Kutembelea Vivutio Vya Utalii.

Mwenyektiti w Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, ,Maliasili na Utalii, Nape Nnauye akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati  hiyo  akiwaonesha kundi la tembo mara baada ya kamati hiyo kufanya utalii nyakati za jioni mwishoni mwa wiki  wakati Kamati hiyo ilipomaliza kufanya  kikao cha kujadili mradi  wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini katika Hifadhi ya taifa ya Ruaha  koani Iringa.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maliasili na Utalii, Neema Mgaya akiwa ameongoza na Mwenyekiti wa Kamati nhiyo, Nape Nnajuye pamoja na wajumbe wengine wakitelemka katika eneo la kuonea wanyama aina ya viboko  nyakati za jioni wanapokunywa maji mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi  wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini. 
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maliasili na Utalii, Mwita Getere akiwa ameongozana  na wajumbe wengine wakipanda ngazi juu ya sehemu ya  kuonea wanyama aina ya viboko  nyakati za jioni wanapokunywa maji mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi  wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja  kwenye jabali ambalo watalii hupanda katika jiwe hilo kwa ajili ya kuona makundi ya wanyama aina ya kiboko wakiwa wanakunywa maji katika mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi  wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini.(Picha na Lusungu Helela-MNRT)


Na.Lusungu Helela - Arusha.- IRINGA
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amewataka Wabunge wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa chachu ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wananchi wanawaongoza  kwa kutenga muda wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Imeelezwa kuwa hamasa ya wananchi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini imekuwa na mwitikio mdogo ukilinganisha na idadi ya watalii wa kutoka nje.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiwa na  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku mbili ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa.

Amesema endapo kila Mbunge kwa nafasi yake ataweza kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii mapato yataweza kuongeza maradufu kupitia Utalii wa ndani tofauti na ilivyo sasa.

"Tengeni muda wa kupumzika baada ya pilikapilika ya kuwahudumia wapiga kura wenu, unakuja huku Ruaha unapumzisha akili huku ukijipanga  mwaka 2020 kwa ajili ya uchaguzi Mkuu" alisema.

" Tusisubiri tuje kikazi kama tulivyokuja hivi, Panga njoo na familia yako ufurahie maisha mara moja moja sio mbaya" Alisisitiza Kanyasu.

Pia, Kanyasu aliwaomba Wabunge hao  kila wanapopata nafasi ya kukutana na wananchi majimboni mwao wawahamasishe kutembelea vivutio vya utalii ili kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa jitihada anazofanya za kutaka kuongeza mapato yatokanayo na sekta ya utalii.

Amesema ufufuaji wa kampuni la usafiri wa ndege nchini (ATCL) kwa kununua ndege saba achilia mbali mradi wa reli ya Standard Garge ni juhudi wazi za  Rais John Magufuli kuona sekta ya utalii inagusa maisha ya kila wananchi kimapato.

Katika hatua nyingine, Kanyasu aliwaomba Wabunge hao wawahamasishe wananchi kuchangamkia fursa za utalii kwa kujenga Hoteli au kwa kuanzishavituo vya  utalii wa kiutamaduni ambao umekuwa ukipendwa sana na watalii wengi wa kutoka nje.

Aidha, Mhe.Kanyasu aliwaeleza Wabunge hao kuwa baada ya kufungua utalii Kusini, Serikali inakusudia kufungua utalii katika kanda nyingine ikiwemo ya kanda ya  ziwa na kanda ya Kaskazini Magharibi, Hivyo wawaandae wananchi wao kuchangamkia fursa za utalii badala ya kubaki walalamikaji.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nape Nnauye alisema kufunguliwa mapema kwa utalii Kusini kutatoa picha halisi kwa wananchi katika kunufaika kiuchumi kupitia sekta hiyo katika kanda nyingine

Pia, Mhe, Nape aliishauri Serikali kulifanyia kazi suala la  tozo ya kuingia ndani ya hifadhi (single entry) kutokana na  malalamiko ya muda mrefu wanayoyatoa wananchi kwanaoishi Katibu na Hifadhi kuwa imekuwa ikiwabana watalii kutoka nje ya Hifadhi kuwatembelea wananchi hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.