Habari za Punde

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akutana na Ujumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi Katika Utumishi wa Umma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 24, 2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi  katika Utumishi wa Ummam, kwenye  Makazi ya Waziri  Mkuu jiji Dar es salaam, Januari 24, 2019. Kutoka kushoto ni  Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula, Mjumbe wa Bodi, George Mlawa na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya  Mishahara na Maslahi  katika Utumishi  wa Umma, George Mlawa baada ya mazungumzo na wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 24, 2019. Wengine kutoka kushoto ni  Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa  amekutana na kufanya mazungumzo wa wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma na ameitaka ifanye kazi kwa weledi.

Ameiagiza ifanye marekebisho ya maslahi kulingana na mazingira ya mtumishi, akitolea mfano kada za elimu, afya, kilimo na mifugo ili yalingane na kazi wanazozifanya.

Amekutana na wajumbe wa bodi hiyo leo (Alhamisi,Januari 24, 2019) katika kikao kilichofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Serikali ina nia njema ya kuhakikisha mishara na maslahi ya watumishi wa umma nchini yanaboreshwa, hivyo ameiagiza bodi hiyo ifanye kazi kwa bidii.

Amesema Serikali imeunda bodi hiyo ili kupata ushauri utakaotokana na tathmini sahihi ya nini Serikali inatakakiwa kufanya ili kuboresha utendaji wa watumishi wa umma nchini.

Serikali inaimani kubwa na wajumbe wote wa bodi hiyo kutokana na uzoefu walionao kwenye  utumishi wa umma.

“Tunataka muongozo mzuri wa kuwafanya watumishi wa umma wafanye kazi yao kwa waledi bila ya kuwa na vishawishi vya aina yoyote ikiwemo kuomba na kupokea rushwa.”


Amesema Serikali inataka kila mtumishi wa umma anawajibika ipasavyo katika kuwatumikia wananchi mambo ambayo yatakuwa yameimarishwa kutokana na upatikanaji wa maslahi mazuri.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.