Habari za Punde

ZURA yatangaza bei mpya za mafuta zitaanza 08/01/19

Na Mwashungi Tahir          Maelezo       
Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia siku ya  Jumanne tarehe 08-01-2019  .
Akizungumza na waandishi wa habari huko kwenye ukumbi wa Maisara Khuzaimt Bakar Kheir kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Maji na Niashati (ZURA) wakati akitoa tarifa kwa umma juu ya mabadiliko ya bei za mafuta zitakazoanza kutumika kuanzia kesho tarehe 8-1-2019.
Amesema sababu za mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi wa Desemba ni kwamba bei za mafuta katika soko la Dunia zimeshuka . Mafuta ya Petroli yaliyosafishwa katika soko la Dunia kwa mwezi wa Novemba , 2018 yameshuka kwa Dola za Marekani 137.07 ikilinganishwa na mwezi wa O         ktoba 2018.
Pia alieleza kwamba Mafuta Dizeli yaliyosafishwa katika Soko la Dunia ka mwezi wa Novemba 2018 yameshuka kwa Dola za Marekani 115.31 ikilinganishwa na mwezi wa Oktoba  , 2018 ambapo mafuta ya Taa (Jet A-1/Keresone ) yaliyosafishwa katika soko la Dunia kwa mwezi wa Novemba 2018 yameshuka kwa Dola za Marekani 96.14 ikilinganishwa na mwezi wa Oktoba 2018.
Aidha alisema aina ya mafuta ya Petroli  Bei ya mwezi wa Desemba , 2018  TSHS  2,459 kwa lita  ambapo bei ya mwezi wa January 2019 TSHS 2,320 kwa lita tofauti TSH 138.87 sawa na asilimia 5.65%.
Kwa upande wa Dizeli  bei ya mwezi wa Desemba , 2018  TSHS 2,539 kwa lita ambapo bei ya January, 2019 2,333 kwa lita tofauti TSH 206.31 sawa na asilimia 8.13%.
Alisema kwenye mafuta ya Taa  bei ya mwezi wa Desemba , 2018 TSHS 1,947 kwa lita  ambapo bei ya January 2019   TSH 1,787 kwa lita tofauti SHS 160.15 sawa na asilimia 8.23%.
Vile vile kwa upande wa mafuta ya Meli (BANKA) bei ya mwezi wa Desemba , 2018 TSHS 2.367 kwa lita  ambapo bei ya mwezi wa January , 2019 TSHS 2,160  kwa lita  tofauti TSH 206.31 sawa na asilimia 8.72%.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.