Habari za Punde

CHANZO CHA MTO LUWEGU

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Namtumbo mara baada ya kuwasili Wilayani hapo kwa lengo la kubaini changamoto za kimazingira na kuweka mikakati ya kuhifadhi Ikolojia ya Vyanzo vya Maji.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akitoka kukagua chanzo cha Maji cha Mto Luegu kilichopo katika Kijiji cha Ngwinde, Kata ya Litola Wilaya ya Namtumbo. Chanzo Mto Luegu kinachangia asilimia 19 ya Maji katika Mto Rufiji. Katika ziara yake Wilayani Namtumbo, Mheshimiwa sima amesisitiza uhifadhi endelevu katika eneo hilo ili chanzo hicho kisivamiwe kwa shughuli za kibinadamu. 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Waziri Mussa Sima akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme vitambulisho maalumu vya wakaguzi wa Mazingira vilivyotolewa na Ofisi yake kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004. Vitambulisho hivyo maalumu vitawezesha wakaguzi wa mazingira kutekeleza majukumu yao kifanisi ikiwa ni pamoja na kusimamia uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira. Makabidhiano hayo yamefanyika hii leo Mkoani Ruvuma.
Picha na Lulu Mussa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.