Habari za Punde

Naibu Waziri Mpya wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe. Simai Mohammed Said Akabidhiwa Ofisi.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa Sasa ni Waziri wa Wizara ya Kilimo Maliasi Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Mmnga Mjengo Mjawiri, akikabidhi dhana za utendaji Kazi kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohamed Said, kulia, hafla hiyo imefanyika katika Majengo ya Wizara hiyo Mazizini Zanzibar.

Waziri wa Kilimo, Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri amewataka watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuwa na mashirikiano mazuri na Naibu Waziri mpya wa Wizara hiyo Mhe Simai Mohamed Said ili kuendeleza sekta ya Elimu nchini.

Akizungumza katika hafla ya kumkabidhi ofisi Naibu Waziri huko Mazizini mjini Unguja, amesema mashirikiano yao yataweza kuibua mafanikio mengine katika sekta hiyo.
Nae Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe Simai Mohamed Said amesema utendaji kazi unazingatia maadili na uwajibikaji hivyo mashirikiano ya pamoja nayo pia yatawezesha Wizara hio kufikia malengo yake iliyojipangia.
Aidha amewataka watendaji wakuu wa Wizara hiyo kutoa taarifa zenye usahihi ambazo zitasaidia katika kufanikisha uwasilishaji bora wa utekelezaji katika vikao vyao vijavyo vya bajeti ya Serikali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.