Habari za Punde

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohamed Said Azindua Jumuiya ya Ushirikiano wa Zanzibar na Ufaransa

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Saidi , akikata utepe kuashiria kufungua Ofisi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Zanzibar na Ufaransa Zanzibar katika jengo la Old Dispensari Malindi Zanzibar kushoto Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bw. Frederic Clavier

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Mohammed Said amewataka wazanzibar kutumia fursa zinazotokea katika kujifunza lugha mbalimbali hasa lugha ya kifaransa ili waweze kutambua lugha mbalimbali za mawasiliano nchini.

Akizundua Jumuiya ya Ushirikiano wa Zanzibar na Ufaransa amesema ili Zanzibar iendelee zaidi ni vizuri kutambua lugha kwani inaweza kuwasaidia pia katika masuala ya ajira ndani na nje ya nchi.

Amesema kuwepo kwa kituo hicho ni fursa pekee kwa wazanzaibari hasa vijana kuweza kujifunza lugha ya kifaransa na kukuza utamaduni wao na kukieneza Kiswahili kimataifa.

Aidha Mhe. Simai ameutaka uongozi wa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kuanzisha matamasha na sherehe mbalimbali za Taifa lao ndani ya Zanzibar ili kukuza mashirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Nae Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bw. Frederic Clavier amesema mashirikiano ya Nchi mbili hizo yatapelekea kuongeza idadi ya watalii Zanzibar na kupelekea kukuwa uchumi wa nchi.

Amesema kwa kupitia Jumuiya hiyo watahakikisha wanakuza lugha ya Kiswahili na Kifaransa kwa lengo la kuwaelimisha vijana kujua lugha hiyo ili waweze kujiajiri na kuajiriwa.

Nae Rais wa Jumuiya hiyo Bw. Said Khamis amewataka vijana wa Kizanzibar kuichangamkia fursa hiyo ili waweze kujiajiri na kuondokana na  utegemezi.

Hata hivyo amesema uzinduzi wa jumuiya hio unaenda sambamba na maonesho ya wiki moja ambapo wasanii mbalimbali watashiriki katika kuonesha fani zao.

Katika uzinduzi huo Naibu waziri Wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe Simai Mohammed Said alipata nafasi ya kuchora Picha kama ni ishara ya kuzindua jumuiya hiyo.







No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.