Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijibu hoja za
wabunge wakati wa kuhitimisha mjadala wa
hoja zilizotolewa kwa wabunge wakati wakichangia makadirio ya mapato na
matumizi ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza
umuhimu wa waandishi wa Habari kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu
yao ya kila siku ili kulinda tunu za Taifa leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Waziri
wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wake Mhe. Juliana Shonza mara baada ya kupitishwa
kwa bajeti ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.
Watendaji
wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Bi Susan Mlawi wakifuatilia majadiliano ndani ya ukumbi wa ubunge
leo kabla ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2019/2020.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.
Kangi Lugola akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kushughulikia
makosa ya jinai ikiwemo kufanya
uchunguzi dhidi tuhuma husika na kubaini ukweli.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisisitiza kuhusu utaratibu unaotumiwa
na Shirika la Fedha Duniani kutoa taarifa ya hali ya uchumi kwa nchi wananchama
Leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifurahia jambo na Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa
Wizara mara baada ya kupitishwa kwa
Bajeti ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo
kwa sehemu ya wasanii leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mmoja
wa wasanii akimpongeza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.
Harrison Mwakyembe mara baada ya
kupitishwa kwa bajeti ya Wizara hiyo leo Jijini Dodoma.
(Picha
zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)
No comments:
Post a Comment