Habari za Punde

Man City 6-0 Watford: Raheem Sterling alifunga hat-trick katika fainali ya kombe la FA

Raheem Sterling alifunga hat-trick ya kwanza ya fainali ya FA tangu 1953 huku Manchester City ikikamilisha msimu mzuri kwa kuicharaza Watford katika uwanja wa Wembley ili kushinda mataji matatu ya ligi ya Uingereza.
Sterling alikuwa nyota wa mechi hiyo huku timu hiyo ya Guardiola ikiwa ya kwanza nchini Uingereza kuafikia malengo ya kushinda taji la ligi, FA na kombe la Carabao kwa msimu mmoja.
Walithibitisha msimu wao mzuri kwa kuiadhibu Watford ambayo iliwachwa bila jibu katika kipindi chote cha mchezo.
Nafasi nzuri ya Watford ya kubadilisha matokeo ilikuja mapema wakati kipa wa City Ederson alipookoa katika miguu ya Roberto Pereyra na walikasirika wakati refa Kevin Friend alipokataa kukubali penalti baada ya Vincent Kompany kuzuia mkwaju wa Abdoulaye Doucoure.
Lakini mechi hiyo ililikuwa imekamilkika wakati David Silva alipofunga akiwa karibu na lango baada ya dakika 26 , huku naye Sterling akifunga goli la pili kabla ya kipindi cha pili kupitia krosi iliopigwa na Gabriel jesus.


Watford walitekeleza mashambulizi baada ya kipindi cha kwanza lakini walizuiliwa.
Waliadhibiwa na kikosi cha City huku mchezaji wa ziada Kevin De Bryune akifunga kutoka kwa pasi ya Gabriel Jesus kabla ya raia huyo wa Brazil kufunga goli jingine muda mfupi baadaye.
Sterling aliandikisha jina lake katika historia ya kushinda mataji matatu katika dakika 10 za mwisho-akifunga pasi ya Bernado Silva kabla ya kuongeza bao lake la tatu katika mchezo uliowafurahisha mashabiki wengi wa City duniani.
Ulikuwa ushindi wa sita wa City katika kombe la FA na wa kwanza chini ya Guradiola ambaye sasa ameshinda mataji sita tangu achukue ukufunzi wa klabu hiyo ya Etihad 2016.
Ushindi huo wa City unamaanisha kwamba Wolvehampton Wanderers ambao walimaliza katika nafasi ya saba katika jedwali la ligi ya Uingereza watashiriki katika mkondo wa muondoano wa kombe la Yuropa tarehe 25 mwezi Julai na tarehe mosi Agosti.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.