Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Azungumza na Ujumbe wa WHO na Madaktari wa Kichina,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimianac na Balozi Mdogo wa Chini Anayefanyia Kazi Zake Zanzibar Mhe. Xie Xioawu, alipowasili katika ukumbi wa mkutano Ikulu Zanzibar, wakati wa hafla ya mazungumzo na Ujumbe wa WHO na Madaktari wa Kichina, kushoto Kiongozi wa Ujumbe huo Dr. Dirk Engels na Profesa Robert .C.Spear, alipowasili katika ukumbi wa mkutano. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Profesa Robert C.Spear, kutoka Chuo Kikuu cha California, alipowasili katika ukumbi wa mkutano Ikulu Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo na Ujumbe huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kiongozi wa Ujumbe huo wa WHO na Madaktari wa China Waliosimamia Mradi wa Kupambana na Kichocho Zanzibar, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo kushoto kwa Rais Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mhe. Xie Xiaowu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa WHO na Madaktari wa Kichina, waliosimamia Mradi wa Majaribio ya Mradi wa Kupambana na Kichocho Zanzibar, ukiondozwa na Dr. Dirk Engels wa WHO, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar. 
Madaktari wa Kichina waliosimamia Majaribio ya Mradi wa Majaribio ya Kupambana na Kichocho Zanzibar, wakifuatilia mazungumzo hayo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, yaliofanyika Ikulu Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mdogo wa Chini Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu kushoto na kulia Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.