Habari za Punde

Dhana ya Afya Moja Yaaza Kutekelezwa Kwa Vitendo Mpakani Namanga

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, (Mweye Ushungi), Kulia kwake ni  Waziri Afya wa Kenya, Mhe. Sicily Kariuki, Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega  wakipata maelezo ya matumizi ya moja ya maabara inayohamishika, ambayo inatumika katika  zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani,   katika mpaka wa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga, linalofanyika,  hadi tarehe  14, Juni 2019.
Wataalam wa sekta za Afya wakijiandaa  kumhudumia mgonjwa wa kuigiza wa Homa ya Bonde la Ufa, aliyeigiza kuwa na ugonjwa huo  mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga wakati wa zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani,
Timu ya Dharura ngazi ya Taifa wakipata maelezo  kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Namanga Dkt. Rose Maro, juu ya namna walivyo weza kuwahudumia wagonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa, wakati wa igizo la zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga
Timu ya Dharura ngazi ya Taifa wakipata maelezo  kutoka kwa Mchinjaji kwenye machinjio ya Namanga, Athumani Ibrahim, juu ya namna wachinjaji walivyo ugua Homa ya Bonde la Ufa kwa kuchinja mifugo yenye ugonjwa huo, wakati wa igizo la zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga
Mratibu wa Dawati la Afya Moja Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akifafanua jambo kwa Timu ya Dharura ngazi ya Taifa wakati wa zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani,  leo  mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga
Timu ya Dharura ngazi ya Taifa wakiwasili katika Kituo cha Afya Namanga, ili kupata maelezo ya  namna kituo hicho walivyo weza kuwahudumia wagonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa, wakati wa igizo la zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga 
Wataalam wa sekta  za Afya kutoka mashirika ya Kimataifa wakiwa  katika chumba maalum cha Menejimenti ya Taarifa za zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani,  leo  mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga, 

Na. OWM, Namanga.
Tanzania kwa kushirikiana na Kenya jana tarehe 11 Juni, 2019, wameanza kutekeleza zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, lilofunguliwa jana mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, ambalo linatekelezwa kwa siku nne,  kuanzia tarehe 11 hadi 14 Juni mwaka huu.

Zoezi hilo, linazingatia Dhana ya Afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu. Wataalamu wa sekta hizo leo tarehe 12, Juni, 2019, wameendelea kutekeleza  zoezi hilo kwa kuzingatia Dhana hiyo.

Wataalamu wa sekta za Afya wa Tanzanaia na Kenya, katika makundi tofauti wameweza kutekeleza kwa vitendo kwa kutumia Dhana ya Afya moja katika  kuhakiki matumizi ya maabara zinazohamishika, kutathmini uwezo wa uchunguzi na usimamizi wa wagonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa mpakani, pamoja na kufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mipango ya Dharura ya Taifa na Kanda, Miongozo ya Utendaji katika kukabili na kupunguza madhara ya Bonde la  Homa ya Ufa kwa Wanyama na Binadamu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.