Habari za Punde

Ujenzi wa Mradi wa Jengo la Kituo cha Kurekebisha Tabia Sober House Kidimni Wilaya ya Kati Unguja

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed akitembelea maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha kurekebishia Tabia {Sober House} katika Kijiji cha Kidimni Wilaya ya Kati.
Katibu Mkuu Shaaban akiwataka Wahandisi Wanaopewa jukumu la kujenga Majengo ya Umma kuzingatia Viwango vinavyokubalika kiubora.
 Nd. Shaaban akielezea faraja yake kutokana na jitihada za Wahandisi wa Ujenzi wa Majengo ya Kituo cha Kurekebishia Tabia {Sober House} Kidimni zinazoonyesha muelekeo mzuri wa Ujenzi wa Majengo hayo.
Mshauri Muelekezi wa Ujenzi wa Kituo cha kurekebishia Tabia Kidimni Bwana Mbwana Bakari Juma akielezea hatua zinazochukuliwa za ujenzi wa majengo hayo ikizingatia ubora unaotakiwa Kimataifa.
Wahandisi wa Ujenzi wa Kituo cha kurekebishia Tabia Kidimni wakiendelea na harakatizao za Ujenzi bila ya kukumbwa na changamoto zozote zile.
Muonekano wa haiba ya Jengo la Kituo cha kurekebishia Tabia linavyoonekana kuwa katika hali ya kupendeza.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis OMPR. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Nd. Shaaban Seif Mohammed ameitaka kampuni ya ujenzi ya Alhilal General Trading kuzingatia viwango vinavyokubalika katika hali  inayoridhisha juu ya ujenzi wa majengo ya taasisi za serikali.
Alisema Serikali inapotoa fedha kwa ajili ya kuekeza na kukamilisha miradi  yake hususani miradi ya ujenzi wa majengo inakua na matarajio makubwa  juu ya ukamilikaji wa mipango hiyo.
Katibu Mkuu Shaaban alieleza hayo wakati akikagua maenedeleo ya ujenzi wa kituo cha kurekebisha tabia (Sober House) kilichopo Kidimini wilaya ya kati Unguja.
Alieleza kuwa, katika kipindi kilichopita kumekuwepo kwa changamoto kwa Kamapuni za ujenzi zinazopewa dhamana hiyo kuchelewesha kukamilisha miradi kwa wakati sambamba na kujenga majengo yaliyo chini ya kiwango hali inayopelekea usumbufu kwa serikali kufanya mambo iliyoyapanga.
“Wakandarasi wengi wanapokuja kuomba kazi wanakuwa watiifu lakini mara baada ya kuipata kazi hiyo huwepo changamoto ya kutokamilisha kazi zao kwa wakati na kujenga majengo yaliokuwa chini ya kiwango”. Alilieza Katibu Mkuu Shaaban.
Pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu alielezea kuridhishwa kwake na hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo na amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Alhilal kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya kipindi kilichokubaliwa kwa mujibu wa mkataba ulivyosainiwa.
Aidha  Katibu Mkuu Shaaban alieleza kampuni hiyo kwa vile hakuna changamoto inayowakabili hadi sasa serikali inatarajia muda wa kukamilika kwa mradi huo utapungua zaidi hali itakayopelekea makabadhiano kufanyika mapema bila ya kuchelewa.
Nae mshauri Muelekezi wa mradi huo wa ujenzi Ndugu Mbwana Bakari Juma alisema kutokana na kasi nzuri inayoendele ya ujenzi hakuna hitalafu zitakazokwamisha na kuhaidi kuwa jengo litakamilika kwa mujibu wa makubaliano yaliyoafikiwa awali.
Alisema jengo hilo litakuwa na ghorofa mbili (2) na pale litakapokamilika litakuwa na lifti ya kisasa, Ofisi pamoja miundombinu rafiki kwa watu wenye mahitaji Maalum {ulemavu} itakayowarahisishia kupata huduma bila ya usumbufu.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Alhilal alimueleza Katibu Mkuu kuwa, Kampuni yao imeanza kazi vizuri na hakuna changamoto zinazokwamisha ujenzi huo hali inayowapa moyo kwamba ujenzi utakamilika ndani ya kipindi kilichokusudiwa.
Akizungumzia changamoto zilizojitokeza kwa kampuni nyengine kuchelewa kukamilisha miradi ya serikali na kujenga chini ya kiwango alimuhakikishia Katibu mkuu Shaaban kwamba kampuni anayoisimamia haitoikwaza serikali kwa changamoto hizo zilizojitokeza sehemu nyengine.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.