Habari za Punde

Waliosoma Skuli ya Kidongochekundu watakiwa kuirudisha katika hadhi yake ya awali.

Wananchi wametakiwa kushirikiana katika mambo mema ya kumcha Mwenyezi Mungu na  sio katika katika Uaduwi na Uasi, Wito huo umetolewa huko Skuli ya Sekondari Kidongochekundu na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh .Hassan Othman Ngwali katika futari ya pamoja ilioandaliwa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Skuli ya Kidongochekundu Wilaya ya Mjini. 
Amesema Skuli hiyo imetoa Wanafunzi wengi na baadhi yao wanashika nafasi mbalimbali za Uongozi hivyo ni vyema kushirikiana katika kuijenga Skuli hiyo ili iweze kuwa ya kisasa na kuvutia. 
Aidha amewataka Viongozi wa Umoja huo kufanya ziara za mara kwa mara kuangalia Mazingira ya Skuli hiyo ili kujuwa matatizo yanayoikabili na kuyatafutia ufumbuzi wa haraka.
Mapema akitoa maelezo Katibu wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Skuli ya Kidongochekundu ili kuweka Mikakati Madhubuti itakayoweza kuunganisha nguvu zao kwa pamoja ili kuirudisha Skuli hiyo katika hadhi yake ya Awali.
Mbali na hayo awaomba kuunga Mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kudumisha hali ya Amani na Utulivu iliopo hapa nchini.
Nao baadhi ya Wananchi walioshiriki katika Futari hiyo wameupongeza Umoja huo na umeweza kuwapa mwanga na matumaini ya kuleta maendeleo katika skuli hiyo na Taifa kwa Ujumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.