Habari za Punde

Wananchi Na Viongozi wa Serikali na Vyama Vya Siasa Wakishiriki Katika Maziko ya Dr. Badria Abubakar Gurnah Katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam

Waombolezaji wakiwa wamebeja mwili wa Dkt. Badriya Abubakar Gurnah, 
mke wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Abdallah Juma Mabodi  katika  mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Upanga jijini Dar es salaam  Juni 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la Dkt. Badriya Abubakar  Gurnah, mke wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Abdallah Juma Mabodi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Upanga jijini Dar es salaam Juni 23, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na ndugu na jamaa wa marehemu Dkt.  Badriya Abdallah Gurnah, mke wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Zanzibar, Abdallah Juma Mabodi  katika mazishi  ya  Daktari huyo yaliyofanyika kwenye makaburi ya Upanga jijini Dar es salaam, Juni 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole, Naibu Katibu Mkuu wa CCM – Zanzibar, Abdallah Juma Mabodi ambaye amefiwa na Mkewe, Dkt. Badriya Abubakar Gurnah wakati alipokwenda nyumbani kwa wazazi wa marehemu, Mikocheni jijini Dar es salaam Juni 23, 2019 kutoa pole kwa familia. Katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.