Habari za Punde

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Azungumza na Waandishi wa Habari Kuhusiana na Tukio la Msaidizi Injina wa Mv Mapinduzi


Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Ndg.Mustafa Aboud Jumbe, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kujinyoga kwa Mfanyakazi wa Shirika la Meli Zanzibaer Msaidizi Injinia wa Meli  ya Mapinduzi 2 Ndg.Haji Abdalla Khatib mwenye umri wa miaka 55 mkaazi wa mtaa wa Kilima Hewa Mjini Unguja 
Katibu Mkuu Ndg. Mustafa Jumbe amesema marehemu alikuwa fundi umeme wa miaka mingi tangu enzi za meli ya ukumbozi ni mtu muhimu sana katika shirika hilo.
Pamoja na hayo amesema uchunguzi wa kifo hicho unafanyika na tayari jeshi la Polisi limeshaaza kazi hiyo mara moja kwa lengo la kubaini sababu za kifo cha injini huyo kujitowa uhai wake. 
Mwili wa marehemu Haji Abdalla Khatib ukiwa katika gari ya Polisi baada ya kushushwa katika Meli ya MV Mapinduzi iliporejea katika Bandari ya Unguja kukatisha safari yake ikiwa ikielekea Kisiwani Pemba ikiwa katika safari zake za kawaidi
(Picha na Abdalla Omar). 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.