Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Simbachawene Aaza KJazi Baada ya Kuapisha leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mpya wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface  Simbachawene alipowasili Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Julai 22,2019 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe  Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mpya wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface  Simbachawene alipowasili Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Julai 22,2019 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano wa Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene akisaini kitabu kwa ajili ya kuanza kazi rasmi alipowasili Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli JIjini Dar es salaam leo Julai 22,2019 mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Wizara hiyo Ikulu Jijini Dar es salaam.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.