Habari za Punde

Breking News Msaidiziu Ingjinia wa Meli ya Mv Mapinduzi 2 Adaiwa Kujinyonga Wakjati Meli Hiyo Ikiwac Katika Safari Yake Kuelekea Kisiwani Pemba.

Mfanyakjazi wa Shirika la Meli Zanzibar, aliyetambuliwa kwa jina la Haji Abdalla Khatib ni Msaindizi Injinia wa Meli ya MV.Mapinduzi 2, inasadikiwa amejinyonga wakati wa Meli hiyo ikiwa katika safari zake za kawaida leo asubuhi meli hiyo ikitokea Unguja kuelekea Kisiwani Pemba mnamo saa mbili za asubuhi amekutwa akiwa tayari ameshafariki katika meli hiyo na kulazimika kurudi Unguja kushusha mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi na kuendelea na safari yake kisiwani Pemba baada ya kuteremsha mwili wa marehemu.

Mkurugenzi wa Shirika la Meli na Wakala Zanzibar  Ndg. Salum Ahmada Vuai amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo ameeleza kuwa mtu huyu alikuwa katika chumba katika meli hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.