Habari za Punde

Kibweni Saccos Yakabidhi Mabenchi Katika Hospital ya KmKm Kibweni.

Na Kijakazi Abdalla  Maelezo  3/07/2019.
KAMANDA wa kamandi ya Afya wa Hospitali yaKMKM Kibweni Zanzibar Suleimani Makame amesema wako tayari kupokea msaada wowote unaotoka kwa wananchi ambao utaweza kuimarisha huduma za bora za kiafya.
Akizungumza kwa niaba ya Komodoo Hassani Mussa Mzee huko katika hospitali ya KMKM Kibweni wakati akipokea Msaada wa vikalio vya wagonjwa (mabenchi) yalio tolewa na Kibweni Saccos kufuatia wiki ya siku ya vyama vya ushirika duniani.
Amesema msaada huo umekuja wakati muafaka kwa  hospitali KMKM  kibweni kwa vile hivi sasa imeweza kutanuka na  kutoa huduma za kiafya kwa kuwahudumia wananchi wengi zaidi.
Amesema msaada huo watautumia kama ilivyo kusudiwa na Saccos hiyo ili kuweza kuzidisha huduma za afya kwa wananchi.
“msaada huu tutautumia kama ulivyo kusudiwa ili kuona huduma za afya zinazidi kuimarika kwa jamii”,alisema kamanda kamandi suleimani Makame.
Aidha kamanda kamandi huyo aliwataka wana Saccos hiyo kujenga Utamaduni wa kurejesha mikopo kwa wepesi mara tu baada ya kupata mikopo ili na wengine wazidi kufaidika.
Alifahamisha kwamba kurejesha mikopo katika Saccos ni kuifanya saccos isiweze kurudi nyuma kimaendeleo bali nikusonga mbele zaidi.
Nae Mwenyekiti wa Kamati za Mikopo Hawa Seif Amour akisoma risala ya Saccos hiyo alisema Saccos hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ni ukosefu wa jengo lao la Ofisi,Elimu ya ujasiria mali,kasha la kuhifadhia pesa,kompyuta, fotokopi mashine na ucheleweshaji wa ulipaji mikopo.
Nae Afisa  ushirika Magharibi “A” Hassan Ali Mbarouk aliisifu Saccos hiyo kwa kufuata agizo la kanuni namba (7) kati ya(14) ya vyama vya ushirika la kuwajali jamii iliyo wazunguka kwa kuwasaidia michango katika maeneo yao.
Aidha aliwataka wanavikundi vyengine vya ushirika viige mfano kama huo kwani vyama vya ushirika vinawajibu wa kujali jamii yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.