Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe..Balozi Seif Ali Iddi Awataka Wananchi Kutunza Mazingira na Kuotesha Miti Mipya.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  akizungumza na Wananchi na Askari wa Jeshi la Polisi katika uzinduzi wa Mradi wa Maji safi  nyumba za Polisi Mahonda.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Yussuf Masauni akimkaribisha Balozi Seif kuzungumza na Wananchi na Askari wa Jeshi la Polisi katika uzinduzi wa Mradi wa Maji safi  nyumba za Polisi Mahonda.
Jumuiya ya Kiraia inayojishughulisha na masuala ya Vijana Tanzania Yourth Icon ikitiliana saini na Mkandasi Mkataba wa ujenzi wa Tangi ta Maji safi na salama lenye Ujazo wa Lita Laki 1.5 katika Kijiji cha Kitope.
Mwakilishi wa Jumuiya ya Kiraia inayojishughulisha na Masuala ya Vijana {TYI}Abdullah Miraji Othman akibadilishana hati ya Mkataba na Mjenzi wa Tangi ta Maji safi na salama katika Kijiji cha Kitope.
Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha Wananchi waendelee kulinda miti pamoja na kuotesha mengine mipya kwa lengo la kurutubisha Ardhi pamoja na kuongeza vianzio vya Maji vitakavyolinda ustawi wa Viumbe.
Alisema Serikali kwa kushirikiana na Taasisi za Umma, Mashirika ya Nje na Jumuiya za kiraia zinajitahidi kuchimba Visima na kujenga Matangi ya kuhifadhi Maji lakini huduma hiyo inaweza kutoweka endapo baadhi ya Watu wataendeleza tabia ya kukata miti onvyo.
Akizindua Mradi wa Maji safi na Salama uliofadhiliwa na Taasisi ya Kiraia ya Direct Aid hapo katika Nyumba za Makaazi ya Jeshi la Polisi Mkoa Kaskazini Unguja zinazomaliza kujengwa katika eneo la Mahonda Balozi Seif alisema wapo baadhi ya Watu wanaoshindwa kuthamini umuhimu wa Miti ambao ni uhai wa Viumbe.
Balozi Seif alisema Jamii inapaswa kuelewa kwamba Miti ina faida nyingi ikiwemo kuweka haiba Nchini ya Nchi, kuongeza Rutba, kuleta Upepo unaopelekea kupatikana kwa Mvua ambayo ni vianzio muhimu vya Maji yanayotumiwa na Viumbe kwa shughuli mbali mbali.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizishukuru na kuzipongeza Taasisi za Kiraia za Direct Aid na TanzaniaYourth Icon zilizojitolea kuisaidiana na Serikali katika kujenga Miundombinu ya uimarishaji wa Sekta ya Maji katika kuwaondoshea shida Wananchi walio wengi hasa wanaoishi Vijijini.
Balozi Seif alisema ushirikiano huo unapaswa kupigiwa mfano kwa vile unakwenda sambamba na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 iliyonadi ya kuahidi kuwapatia Huduma za Maji safi na Salama Wananchi wake wote Nchini.
Akizungumzia Nyumba za Makaazi ya skari wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema uamuzi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa Kujenga Nyumba hizo umelenga kuwaondoshea changamotoya Makaazi inayowakabili inayowakabili Askari hao.
Alisema mfumo wa Askari hasa wale wa Jeshi la Polisi kuishi Mitaani katika nyumba za kukodi hutoa fursa kwa Jamii kuwazoea Askari hao kwa ukaribu unaojengeka jambo ambalo huwepo muhali katika kuchukuwa hatua za Kisheria dhidi ya Watu wanaokabiliwa na Makosa.
Balozi Seif  alimuahidi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar italifanyia kazi Ombi alilolitoa la kutaka SMZ kusaidia nguvu za uwezeshaji katika kuona Nyumba za Makaazi ya Askari wa Jeshi hilo zilizopo Kisiwani Pemba zinamalizika kujengwa.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kiraia ya Direct Aid Bwana Iman Mohammed alisema Taasisi yao itaendelea kushirikiana na Serikali katika azma yake ya kusaidia huduma za Kijamii Nchini.
Bwana Iman alisema Taasisi hiyo ambayo hapo kabla ilikuwa ikijuilikana African Muslim Agency tayari imeshajenga Visima Vitatu katika maeneo ya Mwanakwerekwe palipozana cha kwanza kwa sababu ya mafuriko ya Mvua, Mwera pamoja na cha Mahonda.
Alisema kazi hizo zimekwenda sambamba na kuwasomesha Mayatima mbali mbali wakiwemo Vijana 65 wa Kundi hilo la Mayatima waliokwishamaliza mafunzo ya Chuo Kikuu.
Bwana Iman Mohammed alifahamisha kwamba miradi hiyo iliyolenga kuhudumia Jamii ya Wazanzibari imeshagharimu jula ya Dola za Kimarekani Laki 5.4 sawa na Fedha ya Tanzania Shilingi Bilioni 1.2.
Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Jumiya ya Kiraia inayojishughulisha na Masuala ya kuwaendeleza Vijana { Tanzania Yourth Icon } Bwana Abdullah Miraj Othman alisema Taasisi yao imemua kujenga Tangi kubwa la kuhifadhia Maji safi na Salama Lita Laki 2.5 katika eneo la Kitope ili kuwapunguzia shida ya huduma hiyo zaidi ya Wananchi 5,000.
Bwana Miraji alisema mradi huo mkubwa ambao Mkataba wake umetiwa saini kwenye Hafla hiyo ya uzinduzi wa Maji safi na salama katika Nyumba za Makaazi ya Askari wa Jeshi la Polisi unatarajiwa kugharimu jumla ya Shilingi Milioni 90,000,000/- zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo {UNDP }.
Alisema Tanzania Yourth Icon wakati huu imeamua kuelekeza nguvu zake kubwa katika kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi hasa suala la Maji safi na salama na kuacha mfumo wa nguvu hizo kuzielekeza kwenye masuala ya Semina, Warsha pamoja na Makongamano.
Akimkaribisha Balozi kuzungumza na Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na Wananchi wa maeneo zilipojengwa Nyumba hizoza Makaazi ya Jeshi hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Masauni Yussuf Masauni alisema SMT imetenga Fedha Shilingi Bilioni kwa ajili ya kujenga Nyumba Mia 400 za Askari Polisi katika maeneo mbali mbali Tanzania.
Mhandisi Masauni alisema hayo ni Mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwapatia makaazi ya kudumu nay a Kisasa Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Alisema Kisiwa cha Pemba pekee kimepangiwa kujengwa Nyumba 14 kutokana na uhaba mkubwa wa Nyumba za Askari ambapo kwa sasa ukamilishaji wake umekwama kutokana na uhaba wa fedha kwa ajili ya kukamilisha mambo madogo madogo yaliyobakia.
Akigusia amani na Utulivu wa Taifa uliopo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Masauni amewakumbusha Watanzania kwamba bado lile agizo la Serikali la kuzuia Mikutano ya Hadhara liko pale pale na Vyombo vya Dola havitosita kumchukulia hatua za kisheria Mtu au Taasisi itakayojaribu kukiuka agizo hilo muhimu.
Mhandisi Masauni alisema Serikali ilikuwa na nia safi ya kuzuia mikutano hiyo ili kuwata fursa Wnanchi kuelekeza nguvu zao katika Miradi ya Maendeleo baada ya kugundua uwepo wa Baadhi ya Watu kutaka kuvuruga muelekeo wa Wananchi na badala yake wajiingize katika masuala ya uvunjifu wa Amani.
Hata hivyo Naibu Waziri Masauni alikumbusha kwamba ile Mikutano ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi itaendelea katika Majimbo yao ili kuwapa fursa ya kueleza malengo waliyojipangia katika Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Mradi huo wa Maji Safi na Salama uliolengwa kwa ajili ya Familia za Askari watakaoishi kwenye Nyumba za Makaazi ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja zilizopo Mtaa wa Mahonda pia unatarajiwa kufaidisha Nyumba kati ya 100 hadi 130 za Wananchi Wanazunguuka katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.