Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Awasili Zanzibar Baada ya Kumaliza Ziara Maalum Nchini Uingereza.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea Nchini Uingereza kwa ziara maalum. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amerejea nchini leo akitokea Uingereza.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume viongozi mbali mbali wa Serikali, vyama vya siasa pamoja na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd walimpokea Rais Dk. Shein.


Dk. Shein katika safari hiyo, alifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Watendaji wengine wa Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akifurahia jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchini Uingereza kwa ziara maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake Maalum Nchini Uingereza.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.