Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Mhe. Mussa Sima (kushoto)
akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. George Boniface Simbachawene (katikati) katika Ofisi ndogo ya Makamu wa
Rais jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa Ikulu Dar es Salaam. Kulia ni
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Boniface Simbachawene
akikaribishwa na Bi. Elizabeth Mtiganzi katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais
jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa Ikulu Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Boniface Simbachawene
akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (hawapo
pichani) katika Ofisi ndogo Dar es Salaam, mara baada ya kuwa kuapishwa Ikulu
Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mhe. Simbachawene amewataka watendaji
hao kushirikiana kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment