Habari za Punde

Ziara ya Wafanyabiashara wa Tanzania Wakiwa Nchini Brazil Kutafuta Masoko la Biashara na Kuvutia Wawekezaji.

 Ujumbe wa Wafanya biashara pamoja na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mashirika ya serikali kutoka Tanzania ikiongozwa na mkuu wa msafara Balozi Abdulsamad Abdulrahim ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Mafuta na Gesi nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais na watendaji wakuu wa kampuni ya mafuta na gesi ya Brazil Petrobras mara baada ya kumaliza  mazungumzo ya mashirikano kati ya pande hizo mbili. Mazungumzo hayo yalifanyika leo makao makuu ya kampuni hiyo  jijini Rio de Janeiro. 

Petrobras imeonesha nia yake ya kushirikiana na Balozi Abdulsamad kupitia Jumuia ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi (ATOGS) katika kutoa nafasi za kuwajengea uwezo (capacity building) pamoja na kuangalia fursa za masoko ya bidhaa zao na kibiashara. Katika mazungumzo hayo Balozi Abdulsamad alitoa rai kampuni hiyo kuwekeza tena Tanzania na kuiomba kampuni hiyo kuangalia fursa ziliopo Tanzania ikiwemo: Domestic Production and Marketing of Liquefied Natural Gas (LPG); Domestic Manufacturing of LPG cylinders, Retail distribution less expensive gas burners kutokomeza utumiaji wa makaa; Uanzishwaji wa processing plants pamoja na industries for the production of; refined mineral oil, petroleum jelly and grease;  Uanzishwaji wa chemical industries; Maendeleo ya viwanda vya petrochemicals; Uanzishwaji of LNG Projects na Crude oil refining with efficient export facilities. 

Wakati huo huo Balozi Abdulsamad amewaalika kampuni ya Petrobras kuja Tanzania kwenye Kongamano la Mafuta na Gesi tatehe 2-3 October 2019 ili kutoa experience yao kwenye best practice. 

Baaya kikao cha Petrobras, ujumbe huo ulionana na kampuni ya Brazilian Petroleum, Gas and Biofuels Institute (IBP) Iliyoanzishwa zaidi ya miaka 62 iliyopita na ina uzoefu mkubwa katika masuala ya  udhibiti, viwango, masoko, uendelezaji  masoko, utafiti na uendelezaji wa wataalamu wa sekta ya mafuta na gesi nchini Brazil. IBP imelifurahishwa sana kuona juhudi zinazochukuliwa na Balozi Abdulsamad kuwasaida raia wa Tanzania kuhakikisha wanapewa ujuzi, fursa na kujengewa uwezo.

Kampuni ya IPB imeonesha utayari wake wa kusaini mkataba wa Makubaliano (MoU) baina ya Kampuni hiyo na Jumuia ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi nchini (ATOGS) katika nyanja ya kuwajengea uwezo (capacity building), ujuzi wa kiufundi (technical skills), udhamini wa masomo ya mafuta na Gesi (scholarships) pamoja na kushirikiana na kukuza kipaji cha raia wa Tanzania Ikiwemo standardization na certification za inspection services. Mkataba wa Makubaliano (MoU) utatatiwa saini once matayarisho yatakamilika hivi karibuni.

Kind regards


The Honorary Consulate of the Federative Republic of Brazil, Zanzibar     
P.O.Box 605, Zanzibar 






 




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.