Na Mwashungi Tahir Maelezo
Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya mabadiliko
ya bei za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia siku ya Jumatano ya Tarehe 14-08-2019.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Maisara Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano (ZURA) Khuzaimat Bakar Kheir akitoa sababu za mabadiliko ya bei za mafuta kwa Mwezi Agosti 2019 ni kushuka kwa bei za bidhaa hizo katika Soko la Dunia.
Akielezea aina ya mafuta kwa upande wa Petroli bei ya mwezi wa Julai , 2019 lita TSHS 2,338 ambapo bei ya mwezi Agosti , 2019 litaTSHS 2,181 tofauti -157 sawa na asilimia
6.72%.
Mafuta ya Dizeli bei ya mwezi wa Julai, 2019 lita TSHS 2,319 ambapo bei ya mwezi Agosti , 2019 lita 2,221 tofauti -98 sawa na asilimia 4.23%.
Pia Mafuta ya Taa bei ya mwezi wa Julai, 2019 lita TSHS 1,753 ambapo bei ya mwezi Agosti, 2019 lita TSHS 1,675 tofauti-78 sawa na asilimia 4.45%.
Vile vile Mafuta ya Meli Banka bei ya mwezi wa Julai, 2019 lita TSHS 2,145 ambapo bei ya mwezi Agosti, 2019 lita TSHS.2,047 tofauti -98 sawa na asilimia 4.57%.
Hivyo Khuzaimat amesema Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ZURA inawajuilisha wananchi kwamba bei zilizotangazwa ndio bei halali na kuanza kutumika rasmi kuanzia siku ya Jumatano tarehe 14-08-2019.
No comments:
Post a Comment