Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Uhusino wa Jamhuri ya Namibia
na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa SADC aliyemaliza muda wake, Bi.Netumbo
Nandi Ndaitwah, akikabidhi kijiti hicho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Prof.Palamagamba Kabudi katika
kikao cha Mawaziri wa Nchi za SADC Jijini Dar es Salaam.
Na
Mwandishi Wetu, MAELEZO DAR
ES SALAAM 13.8.2019
MWENYEKITI Mpya wa
Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Prof. Palamagamba
Kabudi amezitaka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
kuendelea kushikamana katika Umoja na Mshikamano baina yao ili kujenga
Uchumi
imara na kuleta Maendeleo ya wananchi wake.
Akizungumza katika
hafla ya kukabidhiwa nafasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam, Prof. Kabudi ambaye
pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, alisema
wakati umefika kwa Nchi za SADC kuungana pamoja katika kushughulikia changamoto
zinazojitokeza katika taasisi mbalimbali za kikanda na kujenga msingi imara wa
ushirikiano.
Prof. Kabudi alisema kwa
miaka mingi Nchi za SADC zimekuwa na ushirikiano mkubwa baina yao hivyo wakati
umefika kwa wananchi wa Mataifa hayo kushuhudia manufaa ya ushirikiano huo
yakileta manufaa makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
Aliongeza kuwa
Tanzania kwa upande wake imeendelea kuwa nchi rafiki na mshirika wa karibu kwa
mataifa yote ya SADC kama inavyojidhihirisha katika historia ya mapambano ya
uhuru wa Nchi nyingi za Kusini mwa Afrika, ambapo mataifa mbalimbali yaliweka
kambi kwa ajili ya wapigania uhuru wake katika harakati zao za kudai uhuru
kutoka kwa wakoloni.
“Mwaka huu tunatimiza
miaka 20 tangu kufariki wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Kiongozi shupavu
aliyejitoa pamoja na viongozi wengine wa SADC katika kupigania harakati za
ukombozi wa Afrika, tunapaswa kumuenzi kwa kuhakikisha tunaimarisha umoja na ushirikiano
uliopo kwa maslahi ya wananchi wetu” alisem Prof. Kabudi.
Prof. Kabudi
aliwataka Viongozi wa SADC kuimarisha Umoja kwa kuwa ndiyo silaha kubwa ya
ushindi katika kujenga mazingira bora ya uwekezaji na biashara ndani ya Nchi za
SADC pamoja na kutoa ushirikiano wa karibu zaidi kwa sekta binafsi kwa ajili ya
kuibua na kujenga fursa za uchumi jumuishi.
Naye Katibu Mtendaji
wa SADC, Dkt. Stegomena Tax alisema jumuiya hiyo imekuwa ikitekeleza programu
na miradi mbalimbali ya ushirikiano wa kikanda ndani ya jumuiya hiyo ambayo
tayari imeleta mafanikio makubwa kupitia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa
Jumuiya hiyo ambao umeweza kutumia rasilimali mbalimbali ikiwemo madini na
nishati kwa ajili ya kujenga uchumi jumuishi.
Anaongeza kuwa katika
Mkutano huo wa 39 unaotarajiwa kuhitimishwa na Mkutano Mkuu wa Marais wa Nchi
za Jumuiya hiyo tarehe 17-18 Agosti mwaka huu, Sekretarieti ya Baraza hilo
imeweza kuzindua Baraza la Biashara la SADC ambalo litakuwa chachu ya
kuunganisha sekta binafsi na ile ya umma katika kujenga uchumi jumuishi kupitia
ajenda ya viwanda pamoja na usimamizi wa rasilimali mbalimbali ndani ya jumuiya
hiyo.
Akizungumzia kuhusu
majanga ya kibinadamu ndani ya SADC. Dkt. Tax alisema kati ya Mwezi Machi-April
Jumuiya hiyo ilipata majanga ya kibinadamu katika Nchi za Msumbiji, Malawi na Zimbabwe,
ambapo pamoja na changamoto hiyo Wakuu wa Jumuiya hiyo waliungana pamoja na
kuweza kuzisadia nchi hizo kwa kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo
madawa na vyakula.
Kwa upande Mwenyekiti
wa Baraza hilo anayemaliza muda wake, ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri
wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah alisema Umoja na mshikamano wa
Jumuiya hiyo umeendelea kuimarika kwa kuwa nchi nyingi zimeendelea kuwa katika
hali ya umoja, amani na utulivu.
Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Uhusino wa Jamhuri ya
Namibia na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa SADC aliyemaliza muda wake,
Bi.Netumbo Nandi Ndaitwah, akitopa hutuba yake kabla ya kukabidhi kijiti hicho kwa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania,
Prof.Paramagamba Kabudi katika kikao cha Mawaziri wa Nchi za SADC Jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Uhusino wa Jamhuri ya Namibia
na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa SADC aliyemaliza muda wake, Bi.Netumbo
Nandi Ndaitwah, akikabidhi kijiti hicho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Prof.Palamagamba Kabudi katika
kikao cha Mawaziri wa Nchi za SADC Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Uhusino wa Jamhuri ya
Namibia na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa SADC aliyemaliza muda wake,
Bi.Netumbo Nandi Ndaitwah, akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Prof.Palamagamba Kabudi mara baad ya kukabidhi kijiti hicho katika
kikao cha Mawaziri wa Nchi za SADC Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania,
Prof.Paramagamba Kabudi na Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), akitopa hotuba yake mara baada
ya kukabidhiwa kijiti hicho kutoka kwa Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa
Ushirikiano wa Kimataifa na Uhusino wa Jamhuri ya Namibia, Bi.Netumbo Nandi
Ndaitwah katika kikao cha Mawaziri wa
Nchi za SADC Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt.Stagomena
Tax, akitoa neno la utangulizi kabla ya Makabidhiano ya kiti cha Uenyekiti kati
ya Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Bi.Netumbo Nandi Ndaitwah kutoka Jamhuri
ya Namibia na Mwenyekiti wa sasa Prof.Palamagamba katika kikao cha Mawaziri wa
Nchi za SADC Jijini Dar es Salaam.
Mawaziri
kutoka Nchi wanachama wa SADC, wakiwa
kwenye kikao cha Mawaziri Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania, kikao hicho kilishuhudia kwa Waziri
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi,
kukabidhiwa rasmi Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri kutoka nchi wanachama .
Baadhi
ya Washiriki wa Mkutano wa SADC unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Tanzania Wakiwa kwenye Kikao cha
Makabidhiano ya kiti cha uenyekiti ambapo Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, amekabidhiwa rasmi kiti hicho.
(Picha na Paschal Dotto Idara ya Habari-MAELEZO).
No comments:
Post a Comment