Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Akabidhi Taarifa ya Utekelezaji

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud akikabidhi kwa furaha taarifa ya utekelezaji ya mwaka  2018-2019  ya Mkoa wake kwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri huko Vuga  Ofisini kwake
Na.Bahati Habib -Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Tawala  za Mikoa ,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za S.M.Z.Mhe. Haji Omar Kheri, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud kwa utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi katika kuleta maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar.
Hayo ameyaema katika makabidhiano ya taarifa ya utekelezaji wa Mkoa wa Mjini Magharibi ya mwaka 2018/2019  huko Ofisi za mkoa huo na kufanya ziara ya  kutembembelea miradi ya maendeleo katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya mjini ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo ya Forodhani na Gizenga ili  kuona shughuli za kitalii zinavyoendelea.
Waziri Kheri ametoa agizo  kwa mkuu wa mkoa kupitia kamati ya ulinzi na usalama kuwaondosha mapapasi na wafanya biashara ambao hawana sehemu maalum wala vibali vya kuendesha shughuli za kitalii katika maeneo ya mji mkongwe ili kupunguza vitendo viovu wanavyofanyiwa wageni.
Wakati huoho muheshmiwa Waziri ametembelea soko jipya la kisasa la machinjio ya kuku linaloendelea kujengwa katika maeneo ya darajani na kuwataka baraza la Manispaa kusimamia usafi wa Soko hilo litakapoisha ili liwe soko la kimataifa.
Nae msaidizi Mkurugenzi Idara za Maendeleo na huduma za kijamii Ndg. Mzee Khamis Juma amesma soko hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi kuku walio hai mia tatu ,  kuku waliochinjwa , sehemu ya machinjio  , sehemu ya kusafishia kuku na sehemu ya kuhifadhia kuku waliobaki baada ya mauzo.
Aidha Waziri amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mjini maghariribi ifikapo tarehe mosi September gari zote zilizopo katika kituo cha daladala  michenzani na kisiwandui kuzihamishia katika eneo la kituo kipya cha kijangwani ili kuondosha msongamano wa gari katika maeneo hayo.
 Pia katika ziara hiyo ametembelea kituo cha afya cha mpendae na kuona huduma zinazoztolewa na kituo hicho ikiwemo huduma za utrasaund kwa mama waja wazito , huduma za kuzalisha na huduma za kungoa meno, sambamba na kuabidhi vifaa kwa ajili ya matumizi ya kituo hicho venye thamani ya milioni kumi na nne.
Aidha amewataka walimu pamoja na kamati za shule kutekeleza    sera  ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.  Ali Mohamed Shein,ya elimu bure kwa   kutokuchangisha mchango wowote kwa mwanafunzi na kuahidi   kuwa ifikapo mwaka 2020 hakutakuwa na mwanafunzi wa shule za msingi   atakaekuwa anakaa chini katika shule zote za Serikai ya Mapinduzi ya  Zanzibar pamoja na kupatiwa madaftari kwa wanafunzi wote  wa shule za msingi za Zanzibar..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib  Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud  kushoto wakitembelea eneo la Darajani wakati wa ziara yake iliofanyika katika Mkoa huo kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama Ndg. Talib Ali Talib. 
Mashine ya kusafishia Kuku(kunyonyoa) aliyoiona Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud (hawapo Pichani) wakati wa Ziara yao huko Soko la Machinjio ya Kuku Darajani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri akimkabidhi moja ya kifaa cha kuchunguzia Ugojwa wa Malaria Daktari Dhamana wa Hospitali ya Mpendae Hamadi Ali katika Hospitali hiyo..
Mwalimu Mkuu Skuli ya Kidongochekundu Msingi “B” Safia Abdul-zakaria Milinga wa kwanza ( Kulia) akisoma Risala mbele ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed kuhusu changamoto na mafanikio ya skuli hiyo.
                                     Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.