Habari za Punde

Nchi 60 Kushiriki Maonesho ya Utalii Tanzania.

Na. Eric Msuya -  MAELEZO 21. 08. 2019.                                                     
Zikiwa zimebaki siku 57 kufikia Tamasha kubwa la utalii hapa Nchini linalofahamika kama “Swahili International Tourism Expo” ,Bodi ya utalii Tanzania TTB imethibitisha kuwa imejipanga vema kuwapokea wageni toka nchi 60 watakaoshiriki Tamasha hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaamleo , Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii,Bi. Devotha Mdachi ameeleza kuwa Tamasha hilo litafanyika oktoba 18 hadi 20 mwaka huu, katika Kumbi za Mikutano Mlimani City, huku mawakala zaidi ya 200 wakitarajiwa kushiriki katika Maonyesho hayo.

Hata hivyo, Devotha amesema juhudi za kufanikisha ujio wa wageni hao zaidi ya 200 kutoka Nchi 60 zimefanywa kwa ushirikiano mkubwa kutoka Bodi ya Utalii TTB pamoja na Balozi zetu mbali mbali za nje.

“mpaka sasa tumepokea uthibitisho kutoka ofisi za ubalozi; toka nchi mbali mbali zikiwemo Ubalozi wa Sweden, Ubalozi wa Tanzania Nchini Malaysia, Ubalozi wa Tanzania Nchini China, Ubalozi wa Korea ya Kusini,  Ubalozi wa Japani, Ubalozi wa Canada, Ubalozi wa Afrika Kusini, Ubalozi wa Omani, Ubalozi wa India,  Ubalozi wa Uingereza,  Ubalozi wa Brazili” Amezitaja Mkurugenzi Devotha.

Akieleza zaidi juu ya upokeaji wa wageni hao watakaofika katika Tamasha hilo, amesema wamejipanga na kujiboresha zaidi kwa kuwapeleka katika maeneo mbali mbali ya utalii nchini, ikiwemo Hifadhi ya Wanyama Serengeti, Uduzungwa, Mikumi, Fukwe za Tanga, Mapango ya Amboni, Mlima Kilimanjaro, Miradi ya Utalii wa Utamaduni mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, pia visiwa vya Zanzibar na Mafia.

Sambamba na hilo, kampuni na Mashirika mbali mbali zaidi ya 30 yamejitoleza kuunga mkono juhudi hizo zinazofanywa na TTB katika kuelekea kilele cha Maonesho hayo.

“kampuni kuu ambazo tayari zimetoa udhaminini  The Global Vector Control Standard, Benki ya CRDB ambayo ni mdau mkubwa katika sekta ya Utalii … pamoja na shirika la Ndege la Ethiopia”

Mkurugenzi alitaja wadhamini wetu wakiwemo ni Air Tanzania … Hifadhi ya Taifa TANAPA, Mamlaka ya Hifadhi ya NgoroNgoro, Mamlaka ya Wanyama Pori Tower, Wakala wa Misitu TFS,na vyama vya Utalii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.