Habari za Punde

Waziri Simbachawene Aendelea na Ziara Yake Kisiwani Zanzibar Kutembelea Miradi ya Upandaji wa Mikoko Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene akizungumza na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais alipotembelea mradi wa upandaji mikokoko katika  Shehia ya Kilimani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Magharibi.
Mratibu wa Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Khalid Bakari Hamrani (kushoto) akimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene kukagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kianga katika Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene (wa pili kulia) akiendelea kutembelea mradi wa ujenzi wa akituo cha afya Kianga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene (mbele katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud (wa pili kulia),Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mihayo Juma Nunga (wa pili kushoto), Katibu Mkuu Ofisi hiyo Shaaban Seif (kulia) pamoja na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene (katikati) akiangalia maabara ya kituo cha afya Kianga alipofanya ziara Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wanaosimamia mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Kianga pamoja na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Muungano na Makamu wa Pili wa Zanzibar.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.