Habari za Punde

Balozi Seif afungua Tamasha la Pili la Utalii Zanziba akimuwakilisha Rais Dk Shein

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Banda la Kamisheni ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} Kwenye Tamasha la Utalii huko Verde Hoteli Mtoni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ushushaji na upakizi wa Mizogo Uwanja wa Ndege  { ZAT} Mh. Mohamed Raza Hassanali akimpatia maelezo Balozi Seif alipotembelea Banda la Taasisi hiyo
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiangalia ubara wa Bidhaa za anafaka zinazozalishwa hapa Nchini ambazo ziko katika kiwango kinachokubalika kuingia sokoni 

 Balozi Seif akilifungua Tamasha la Pili la Utalii Zanzibar hapo katika Hoteli ya Kimataifa ya Verde Mtoni akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein.
 Baadhi ya Mabalozi wa Nchi mbali mbali waliopo Tanzania  ambao nayo walishiriki Tamasha la Pili la Utalii Zanzibar hapo katika Hoteli ya Kimataifa ya Verde Mtoni.

 Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo akitoa maelezo ya washindi katika Sekta ya Utalii kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kulifungua Tamasha la Pili la Utalii Zanzibar.
 Balozi Seif akimkabidhi Cheti Maalum Bwana Ali Samantari mwenye asili ya Mombasa Kenya kutokana na mchango wake katika Sekta ya Utalii katika harakati za kusafirisha Watalii katika eneo la Afrika Mashariki.
 Balozi eif akimkabidhi Cheti Maalum Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi Muombwa kwa mchango wake katika Sekta ya Utalii wakati akiwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Balozi Seif akiangalia bidhaa zilizotengenezwa kwa Udongo zilizozalishwa na Wajasiri Amali Wazawa na kuvutiwa na kazi yao inayopata soko katika Sekta ya Utalii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.