Habari za Punde

Bodi ya Uhaulishaji Ardhi Zanzibar yafika Shumba Mjini kutoa ellimu

  Sheha wa Shehia ya Shumba Mjini  Rahila Ramadhani Juma  akiwakaribisha  wajumbe wa Bodi ya Uhaulishaji Ardhi Zanzibar waliyofika kisiwani hapo kwa ajili ya kutoa Elimu ya Majukumu katika Bodi hiyo ghafla hiyo iliyofanyika Micheweni  Kisiwani Pemba
 Afisa Utambuzi kutoka Bodi ya Uhaulishaji Ardhi Zanzibar Shawana Sudi Khamis akitowa Elimu kuhusu amjukumu ya bodi hiyo  kwa Wananchi waliyofika Micheweni katika Shehia ya Shumba Mjini Kisiwani Pemba
 Mwananchi kutoka Shumba Mjini akiuliza Swali kwa wajumbe wa Bodi ya  Uhaulishaji Ardhi Zanzibar baada ya kupatiwa  Elimu kwa juu ya majukumu ya Bodi hiyo.
  Mjumbe kutoka Bodi ya Uhaulishaji  Ardhi Zanzibar Masoud Salum Mohamed akijibu masuwali kwa wananchi waliyofika katika Mkutano huo uliyofanyika Micheweni Shehia ya Shunba Mjini Pemba.
 Wananachi wakimsikiliza Afisa Utambuzi  hayupo pichano wakati alipokuwa akitoa Elimu juu ya Majukumu ya Bodi ya Uhaulishaji.
Wajumbe wa Bodi ya Uhaulishaji Ardhi Zanzibar wakifuwatilia Maelezo kwa wajumbe wanaowasilisha Elimu ya Bodi hiyo.
                                              Picha na Miza Othman –Malezo Pemba.

Na Miza Othman –Maelezo Pemba.
Bdi ya Uhaulishaji ndio chombo pekee cha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chenye dhamana ya kuidhinisha aina yeyote ya uhaulishaji wa rasilimali ya ardhi nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Utambuzi wa Bodi ya Uhaulishaji ardhi  Shawana Sudi Khamis wakati alipowapatia Elimu ya  umuhimu wa Uhaulishaji ardhi kijijini Shehiya ya Shumba Mjini .
Amesema ni vyema kijiji hicho  kupatiwa Elimu wananchi hao kwani kutawapelekea manufaa katika jamii zao na kuondokana na migogoro  ya ardhi yanoweza kuepukika kijijini mwao.
Aidha Shawan Sudi amesema  Bodi ya Uhaliashaji  Ardhi  ni bodi yenye haki ya kulinda rasilimali ya ardhi kwa maslahi ya taifa na maendeleo ya jamii kwani kufanya hivyo kutapelekea kulinda kwa haki zote na kuzingatia masilahi  bila ya kuathiri  ya jamii ya Zanzibar.
Nae Mjumbe wa Bodi ya Uhaulishaji Ardhi Masoud Salim Mohammed ameseama kuwa miongoni mwa sababu za msingi zilizopelekea kuanzishwa kwa bodi hiyo ni pamoja na hoja ya kisheria nam 12/1992 ambayo imeekwa wazi hoja ya kuwepo chombo kitakachoshughulikia Uhaulishaji wa ardhi na usajili wake.
Ameeleza kuwa wameamua kuja katika kijiji hicho kutoa Elimu hiyo  ili  Wananchi wafahamu umuhumi wa uhaulishaji ardhi na kuweza kufaidika kupitia njia mbali mbali wakati watakapo jisajili ikiwemo kufanya uhaulishaji wa salama na wauhakika, kuepusha migogoro ya ardhi katika jamii  na Serikali kupata kumbukumbu za uhakika katika uhaulishaji.
 Hata hiyo amewataka wananchi wanaotaka kuhaulisha ardhi zao wanapaswa kuitumia Bodi ya Uhaulishaji ardhi kwa kuwa na uwezo wa kuzilinda rasilimali zao katika jamii na Serikali kwa ujumla.
Wananchi wa Shumba Mjini wameipongea Bodi hiyo kwa kufika hapo na kuwapatia Elimu ya Uhaulishaji ardhi katika kijiji chao kwani ni fursa adhimu  na kuiomba Bodi hiyo isitosheke kutoa elimu na iweendelevu katika utowaji wa elimu hiyo kwa Vijij Vyengine.
Aidha wananchi hao wameiomba Bodi ya Uhaulishaji ardhi kuwapunguzia masafa wakati wanapohitaji huduma katika Ofisi zao na kuwapunguzia ada ya malipo kutokana na kipato duni cha maisha yao.
Sheha wa shehi ya Shumba Mjini ameishukuru Bodi hiyo kwa kuwamuwa kuja kutoa Elimu katika kijiji chake kwani wananchi wa kijji hicho bado hawanamwako wa kujisajili katika bodi hiyo.
Bodi ya Uhaulishai wa Ardhi Zanzibar ilianzishwa rasmi mwenzi wa machi mwaka 2009 chini ya sheria ya Uhaulishaji Ardhi nam 8 ya mwaka 1994 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007 kwa sheria nam 10/ 2007.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.