Habari za Punde

Tamasha la Tamaduni na Sanaa la Nchini za Afrika Mashariki Litumike Kukiuza Kiswahili.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Selemani Jafo akizungumza alipotembelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.


Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa Tamasha la utamaduni na sanaa la nchini za Afrika mashariki litumike kukiuza kiswahili ili na nchini mwanachama wa Afrika Mashariki waweze waongee lugha hii adhimu ambayo sasa ni lugha rasmi katika jumuiya za Afrika.
Amesema hayo alipotembelea maonesho ya Tamasha la Uatamaduni na Sanaa la nchi za Afrika amashariki al-maalufu kama JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwa nja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

"Nimetembelea mabanda mbalimbali na kujionea bidhaa mbalimbali za asili na utamaduni wa maeneo mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki za wajasiriamali wa nchi zote".

Amesema kuwa wizara ya Tamisemi ni chumvi, Afya, elimu vipo chini ya wizara yake, lakini wizara ya habari utamaduni, Sanaa na Michezo hususani Maafisa Utamaduni wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri wako TAMISEMI, hivyo unaweza kuona kwanini yupo hapa.

Hata amewapongeza wizara ya habari na utamaduni kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuhakikisha tamasha hili linafanyika kama lilivyopangwa na kwa mafanikio makubwa hasa kukidhi kiu ya wananchi wanaohudhuria tamasha hili adhimu.

"Sina cha kuficha, nimefurahishwa na mambo yote niliyoyaona hapa uwanja wa Taifa hakina mmejipanga vyema, hongerani sana," amesema.

Pia amesema kuwa amefurahishwa na maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST na amewasihi wananchi kuja kwenda Uwanja wa Taifa kujifunza tamaduni mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.