Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Azungumza na Mawaziri Kuhusiana na Utatuzi wa Ardhi Nchini.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa taarifa kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuridhia misitu ya hifadhi iliyopoteza sifa itolewe kwa mwananchi kwa ajili ya shughuli za Kilimo na Mifugo ili kuwandolea kero za uhaba wa ardhi. Kauli hiyo aliitoa kwenye ukumbi wa Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Septemba 23, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri waliochambua na kuandaa taarifa ya mapendekezo ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi nchini iliyowasilishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri, Septemba 23, 2019. Kutoka kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hasmis Kigwangala, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,  Selemani Jafo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, George Simbachawene, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina na Waziri wa Maji, Profesa, Makame Mbarawa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungmza na Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya pamoja ya Mawaziri nane wa Sekta zinazohusika na Matumizi ya Ardhi iliyoundwa na Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhusu Mapendekezo ya kupata ufumbuzi wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi Nchini. Mkutano uliofanika katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es salaam.
.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.