Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Akiendelea na Ziara Yake Ras Al Khaimah leo.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiwa pamoja na Mhe.Mohammed Ali Musabah,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda wa Ras Al Khaimah wakimsikiliza mtoa Mada inayohusiana na Utalii iliyowasilishwa na Meneja wa Mamlaka ya Maendeleo ya Utalii wa Serikali ya Ras Al Khaimah Bi.Navritu Rai.(hayupo pichani) mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa  Waldorf Astoria Ras Al Khaimah.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika mkutano na  Viongozi  wa Kampuni za Uwekezaji na Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenye Viwanda pamoja na Mamlaka za Vitega Uchumi ya Ras Al Khaimah, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Hotel ya Waldorf Astoria Ras Al Khaimah)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Meneja waMamlaka ya Maendeleo ya Utalii wa Serikali ya Ras Al Khaimah. Bi.Navritu Rai, baada ya kumaliza mkutano na Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Waldorf Astoria Ras Al Khaimah) 
Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.