Habari za Punde

ZIARA YA WAZIRI KAIRUKI KIWANDA CHA KUCHAKATA MAHINDI CHA JKT MLALE.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Kikosi cha JKT 842 Mlale wanaosimamia kiwanda cha kuchakata Mahindi kinachohudumiwa na kikosi hicho wakati wa ziara yake ya kukagua mazingira ya uwekezaji katika mkoa wa kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma
 Kamanda wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi akiwasilisha hotuba yake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki wa kwanza kushoto akifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi wakati wa ziara yake katika kiwanda cha kuchakata Mahindi kinachosimamiwa na kikosi hicho
Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi akiwasilisha hotuba yake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akioneshwa mitambo ya kuchakata mahindi na kusaga unga wa sembe na Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi alipotembelea kukagua namna Kikosi hicho kilivyowekeza katika shughuli za uzalishaji.Kiwanda hicho kipo Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi kuhusu magunia ya pumba za mahindi yaliyohifadhiwa baada ya kuchakata na kutoa unga wa sembe katika kiwanda hicho.
Baadhi ya vijana wa JKT wakiimba wimbo wa kumkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (hayupo pichani) alipotembelea kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Mlale mkoni Ruvuma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akipokea zawadi ya unga wa sembe unaotengenezwa katika kiwanda cha kuchakata mahindi kinachomilikiwa na Kikosi cha JKT Mlale alipotembelea kiwandani hapo 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na vijana wa JKT waliopo katika kikosi cha JKT 842 Mlale wakati wa ziara yake.
Sehemu ya Watumishi wa Serikali waliohudhuria wakati wa ziara hiyo katika kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Mlale wakifuatilia maelezo ya Waziri Kairuki (hayupo pichani).
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.