Habari za Punde

Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Yatembelea Miradi ya Vijana Mkoani Iringa.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara Mkoani Iringa kwa lengo la kukagua miradi ya vijana iliyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. (Wa tatu kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga (Mb).
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa ya Mkurugenzi wa Kiwanda cha EatFresh Bi.  Hadija Jabiry (hayupo pichani), walipofanya ziara Mkoani Iringa kwa lengo la kutembelea miradi ya Vijana iliyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kusindika Mbogamboga na Malimbichi cha EatFresh Bi. Hadija Jabiry (kulia) akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati walipotembelea kiwanda hicho kilichopo eneo la SIDO, Mkoani Iringa.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha EatFresh wakiendelea na kazi ya kuchambua maharage mabichi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga (Mb) akieleza jambo wakati Kamati hiyo ilipokutana na watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa kwa ajili ya kupokea taarifa kuhusu miradi ya vijana iliyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa ya vikundi vya vijana vilivyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (hayupo pichani), walipofanya ziara Mkoani Iringa kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Mfuko huo.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa ya vikundi vya vijana vilivyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (hayupo pichani), walipofanya ziara Mkoani Iringa kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Mfuko huo na kutembelea miradi ya vikundi vya vijana. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Ally Saleh (kulia) akichangia jambo kuhusu miradi itakayowanufaisha watu wenye ulemavu kunufaiaka na Mfuko huo wa Maendeleo ya Vijana.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (wa pili kutoka kulia) akieleza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipofanya ziara ya kutembelea miradi ya vijana iliyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Mkoani Iringa. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga (Mb).
Kiongozi wa Kiwanda cha vijana cha EnviBright Bw. Paul Myovela (kulia) akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria namna wanavyotengeneza mbolea inayotokana na taka ngumu.
Muonekano wa Kiwanda cha EnviBright kinachojihusisha na utengenezaji wa mbolea kupitia taka ngumu.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu 
(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.