Na.Eric Msuya – MAELEZO.
Makamu
wa Rais mama Samia Suluhu Hassan anatalajia kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa 58 wa mwaka wa Shirika la
Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) utako anza Jumatatu tarehe 21 hadi 25 Oktoba jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga, amesema Mkutano huo utaudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa
Serikali kutoka Nchi 48 za Wanachama wa Shirika hilo pamoja na Masharika
mbalimbali ya Kitaifa.
“Mkutano
huu utakaoanza Jumatatu unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri, Wanasheria Wakuu
wa Serikali toka Nchi Wanachama, Wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya
Kimataifa, Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao hapa Nchini na Viongozi Waandamizi
wa Serikali kutoka Nchi Wanachama” Amesema Mhe. Mahiga
Mkutano
huo utaofanyika kwa siku tano, utajadili masuala mbalimbali ya kisheria za
Kimataifa ikiwa pamoja na Changamoto za kisheria zinazoyakabili Mataifa Wanachama
na Kuangalia namna bora ya kushughulikia changamoto hizo ili kuwa na Dunia
yenye Amani, Usalama na Utulivu kwa ajili ya Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa na
Kijamii.
Sambamba
na hilo maswala mengi yatako jadiliwa katika mkutano huo ni, Sheria ya
Kimataifa ya Bahari, Mitandao na Biashara na Uwekezaji, Kuvunjwa kwa Sheria ya
Kimataifa Nchini Palestina, Utatuzi wa Migogoro kwa njia ya Amani, Matumizi ya
Sheria za Nchi nje ya Nchi na Tume ya Sheria ya Kimataifa.
Tanzania
ilijiunga na The Asian – African Legal Consultative Organisation (AALCO) mwaka
1973 chini ya Uongozi wa Rais Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, huku Tanzania
ikiwa ni mara yake ya tatu kuwa wenyeji wa kushiriki katika mkutano huu wa
Shirika la Mashauriano ya kisheria kwa nchi za Asia na Afrika
“Kwa
mara nyingine tena, Tanzania tunakuwa wenyeji kwa mara ya tatu katika mkutano huu
… Nchi yetu ina miaka 46 toka tujiunge na chama hichi, mafaniko ni mengi na
maslahi ni makubwa na mapana tunayoendelea kuyapata katika chama hiki” Amesema
Mhe. Mahiga
Shirika
la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika ( The Asian-
African Legal
Consultative Organisation – AALCO kilianzishwa
mwaka 1956 ikiwa ni matokeo ya Mkutano wa Kihistoria wa Bangung,
Indonesia tarehe 18-24 April 1995 (Bandung Conference).
No comments:
Post a Comment