Wana Kikundi cha Kuweka Akiba cha Tuwe Wakweli kilichopo Muyuni “B” Mkoa wa Kusini wakiwa pamoja na Wasimamizi wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kutoka Tasafa wakisherehekea upatikanaji wa Hisa zilizogaiwa kwenye Hafla hiyo.
Na.Kassim Salum Abdi. OMPR.
Jamii nchini imeshauriwa kuzitambua fursa zilizowazunguka ili ziweze kuwanufaisha kwa ajili ya kuinua kipato chao, familia sambamba na kuongeza Mapato ya Taifa.
Kufanya hivyo kutusaidia kuirahisisha Serikali kuu kufikisha maendeleo ya jamii kwa haraka pamoja na kuleta mabadiliko ya haraka yanayoendana na Sera, Mpango na Mkakati wa kupunguza Umaskini (MKUZA) kwa Taifa.
Mratibu wa Tasaf Unguja Ndugu Makame Ali Haji, ameeleza hayo wakati akizungumza na Kikundi cha Kuweka Akiba cha Tuwe Wakweli kilichopo Muyuni B Mkoa wa Kusini Unguja katika Shughuli Maalum ya kugawana Hisa waliopata kwa mara ya Kwanza tokea kuanzishwa kwa Kikundi hicho.
Mratibu Makame ameridhishwa na kufurahishwa na kitendo cha Kikundi cha Tuwe Wakweli kwa hatua waliofikia ya kuendeleza Mpango wa TASAF jambo ambalo ndio lengo hasa lililokusudiwa la kuendeleza Miradi hiyo mara baada ya Kuachwa kuendelezwa na Wananchi Wenyewe .
Alisema vipo Vikundi visivyofikia lengo la kuendeleza Miradi walionzishiwa na Viongozi jambo ambalo baadae hutoa Changamoto kwa Serikali na Walengwa wenyewe katika Azma nzima ya kujiletea Maendeleo na Kupambana na Hali ya Umaskini.
Aliwashauri Wana kikundi hao Mbali na Kugawana Hisa hizo bado ipo haja ya kubuni Miradi Mengine ya muda mrefu ikiwemo Kilimo na Bidhaa za Baharini hali ambayo itawasaidia kuongeza Mitaji yao na kupata faida zaidi.
Nae Mratibu wa TASAF Zanzibar Ndugu Saida Saleh Adam aliwapongeza akina Mama hao kwa jitihada na Uwaminifu wao uliowafikisha hatua ya Kugawana Hisa kwa kila Mwanachama na kuwataka kuzitumia Fedha hizo kwa Uwangalifu ili ziweze kuwanufaisha badala ya kutumia kwa matumizi yasiyokuwa ya lazima.
Ndugu Saida aliwaeleza wana Kikundi cha Tuwe Wakweli kwamba hatua waliofikia ni ya kuigwa na Vikundi vyengune vilivyopo Zanzibar na aliwaahidi kupitia Mpango huo wa Kupunguza Umaskini Serikali itaendelea kuwapa msukumo zaidi. Hivyo kuna haja ya kujipanga vyema na kuendeleza Uaminifu kama jina lao linavyojieleza.
Akisoma Taarifa ya Kikundi cha Tuwe Wakweli Katibu wa Kikundi hicho Suleiman Mgeni alisema Kikundi chao Kinajishughulisha na Biashara ya Kukopeshana Bidhaa tofauti na kufanikiwa kukusanya Jumla ya Shilingi Millioni Moja Laki Tisa na Thelathini na Tisa Elfu ambazo zitagaiwa kwa Walengwa 14.
Katibu Suleiman alisema kuanzishwa kwa kikundi hicho kumeleta Faida kwa Wanachama wake ikiwemo Kudumisha Hali ya Umoja na Ushirikiano Miongoni mwao, kupatikana kwa uzoefu kwa njia ya Vitendo juu ya kuendesha Biashara pamoja na kupata Uhakika wa kupata Mtaji kwa ajili ya kuendeleza Biashara.
Akigusia Changamoto zinazowakabili Ndugu Suleiman alizitaja ikiwemo Elimu ndogo ya Uendeshaji wa Kikundi Utoro wa Wanachama Kuhudhuria vikao, kuchelewa kwa Ukusanyaji wa His. hivyo walimuomba Mratibu kuzipatia Ufumbuzi Changamoto hizo hasa kwa kupatiwa Elimu zaidi.
Kikundi Cha Tuwe Wakweli Kimeanzishwa mnamo Mwaka 2018 Kikiwa na Jumla ya Wanachama Kimi na Nne (14) Wanawake 13 Na Mwanamme 1.
No comments:
Post a Comment