Habari za Punde

Ujumbe wa Chama cha CPC cha China Wawasili Kisiwani Zanzibar.

 
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha (CPC) Mhe.Guo Yezhou,mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ajili ya ziara ya kuimarisha mahusiano baina ya CPC na CCM.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, akizungumza na ujumbe wa watu watano kutoka Chama cha Kikoministi cha China (CPC), walipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
NAIBU Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha (CPC) Mhe.Guo Yezhou,akivishwa skafu na Vijana Maalumu wa UVCCM baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
NAIBU Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha (CPC) Mhe.Guo Yezhou, akiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar  marehemu Sheikh Abeid Amani Karume hapo Kisiwandui Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, akimuonyesha picha ya jengo la Chama Cha Mapinduzi na Mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha (CPC) Mhe.Guo Yezhou. 
NAIBU Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha (CPC) Mhe.Guo Yezhou(kulia, akimkabidhi zawadi Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi (kushoto).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.