Habari za Punde

Uongozi wa PBZ watakiwa kufanyia marekebisho miundo mbinu ya kukabiliana na maafa

Takdir Suweid, Zanzibar.                     
Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) umetakiwa kuyafanyia marekebisho ya mapungufu yaliopo katika Miondombinu ya kukabiliana na Maafa ili kulinda Maisha ya Watu na Mali zao wakati Majanga yanapojitokeza.
Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya kukabiliana na Maafa Zanzibar Makame Khatibu Makame wakati wa ziara ya kushtukiza ya kuangalia Miondombinu rafiki ya kukabiliana na Maafa katika Banki Tawi la Mwakwerekwe na Malindi.
Amesema suala kuwepo Milango ya dharura,Milango inayofunguka kwa pande zote mbili,Mazingira rafiki kwa Watu wenye ulemavu na kuweka maeneo maalum ya uokozi ni muhimu katika Banki hiyo.
Aidha amesema lengo la kufanya ziara hiyo si kuwakomoa Viongozi na Watendaji wa Banki hiyo bali ni kuangalia jinsi ya kukabiliana wakati Majanga yanapojitokeza.
Kwa uapande wake Naibu Mkurugenzi wa PBZ Mtendaji Khadija Shamte ameahidi kutoa mafunzo ya kukabiliana na Maafa kila mwaka na kuweka Miondombinu rafiki japo kuwa ni vigumu kwani baadhi ya Matawi wanatumia ya kukodi lakini watajitahidi kutekeleza,Sheria,Kanuni na Miongozo iliowekwa ili kulinda Wananchi na Mali zao

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.