Na
Mwandishi Wetu
BARABARA
ya kutua na kuruka ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Arusha itaongezwa urefu, ili
iweze kuruhusu ndege kubwa za abiria kuanzia 70 ziweze kutua na kuruka bila tatizo,
imeelezwa.
Mhe.
Husna Malima, Mbunge wa Kigoma Kusini mwishoni mwa juma hili (Ijumaa) alihoji Je serikali inampango gani wa
kuboresha Kiwanja cha Ndege cha Arusha ili wananchi wa mikoa ya Singida,
Manyara, Simiyu, Manyara, Mara na Dodoma wahamasike kutumia usafiri wa ndege,
ambazo zinatosheleza kwa sasa?
Amesema
mafaniko ya uwepo wa ndege nyingi za abiria nchini ni pamoja na ndege hizo
kutumika kwa wananchi kuzipanda.
Akijibu
swali hilo Bungeni, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Issac
Kamwelwe amesema kurefushwa huko kutafanikisha ndege aina ya Bombardier ambayo
inabeba abiria kuanzia 70 kutua na kuruka bila tatizo.
Mhe.
Kamwelwe amesema tayari bajeti imetengwa kwa ajili ya kazi hiyo, ambapo kiwanja
hicho ni cha tatu nchini kwa kutua na kuruka ndege nyingi zaidi ya 125 kwa
siku.
“Tumeweka
bajeti kuendeleza kiwanja cha ndege cha Arusha na tayari tenda imetangazwa,
kiwanja hiki kinaongoza kwa kutua ndege nyingi zaidi kwa siku ni biashara kubwa
na ndio maana tunataka ndege ya Bombardier itue hapo,” alisisitiza Mhe.
Kamwelwe.
Amesema
mikoa jirani na Arusha ya Manyara, Singida, Dodoma, Simiyu na Mara itafaidika
na maboresho ya kiwanja hicho kwa kuwa wataweza kukitumia ipasavyo.
Naye
Meneja wa Kiwanja hicho, Mhandisi Elipid Tesha amesema barabara ya kutua na
kuruka ndege itaongezwa urefu kwa meta 200, ambapo sasa inaurefu wa meta 1600
na itakuwa 1800, na pia patajengwa eneo la kugeuza ndege.
Mhandisi
Tesha amesema kwa sasa kazi inayoendelea ni ujenzi wa eneo la maegesho ya ndege
(Apron), ambayo yakikamilika yatapunguza msongamano kwa asilimia 30; pia barabara
ya kupita ndege kwenda katika maegesho (taxiway); ujenzi wa maegesho ya magari yapatayo 350 kwa
kiwango cha lami ambapo unakwenda sambamba na ujenzi wa mfumo wa malipo ya
maegesho hayo.
Pia
amesema ujenzi huo wa maboresho ya kiwanja cha ndege cha Arusha utahusisha
ujenzi wa eneo la kupumzika abiria, ofisi za waegesha ndege (mashellers),
kibanda cha ulinzi na vyoo .
No comments:
Post a Comment