Habari za Punde

Dk.Shein Aridhishwa na Mafanikio Makubwa Yaliopatikana Zanzibar Chini ya Uongozi Wake.wa Awamu wa Saba na Kutimiza Miaka Tisa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akijibu suala wakati wa mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar Ndg,Chande Omar Omar yanayohusu miaka tisa ya Uongozi wake,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]02/11/2019.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuridhishwa na mafanikio makubwa yaliopatikana Zanzibar chini ya uongozi wake wa Serikali ya Awamu ya Saba ambao umetimiza miaka tisa.

Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) Chande Omar Omar kufuatia kutimiza miaka tisa ya uongozi wake wa kuiongoza Zanzibar.

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alisema kuwa anafurahia miaka tisa ya uongozi wake kutokana na mafanikio makubwa yaliopatikana hapa Zanzibar ambayo kwa kiasi kikubwa yametokana na kutekeleza mambo ya msingi ikiwemo kutekeleza  Ilani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015 na 2015-2020.

Aliongeza kuwa Serikali inatakiwa baada ya kumaliza uchaguzi wake chama kilichoingia madarakani kinatakiwa kutekeleza ahadi zake jambo ambalo ndilo lililofanywa na Serikali anayoiongoza ambayo imetekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi ilizoahidi ndani ya kipindi cha miaka tisa ya uongozi wake.

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa amefurahi kuona kwamba katika uongozi wake mafanikio makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa MKUZA II alioanza nao na MKUZA III unaondelea hivi sasa.

Alieleza ni kuendeleza Alieleza kuwa Serikali anayoiongoza imeendeleza umoja na mshikamano mkubwa wa wananchi wa Zanzibar kwa kutambua kuwa bila ya kuwepo kwa umoja na mshikamano huo hapatakuwa na maendeleo endelevu.

Alisisitiza kuwa azma ya CCM ni kutekeleza umoja na mshikamano na ndio maana katika kipindi chote cha uongozi wake wa miaka tisa ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Zanzibar umeimarika.
Alieleza kuwa Serikali zote mbili ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kusimamia amani na usalama uliopo nchini na kusisitiza kuwa ndani ya miaka tisa ya uongozi wake nchi imekuwa salama.

Rais Dk. Shein alieleza kuwa sekta nyingi za maendeleo zimeimarika katika kipindi cha miaka tisa cha uongozi wake  ulinzkatika katika uongozi wake Serikali imetekeleza kwa kiasi kikubwa shughuli za kijamii zikiwemo huduma za afya, elimu, suala zima la kuangalia hali za wananchi pamoja na shughuli za maendeleo zimeimarika.

Alisema kuwa kila sekta imeweza kupata mafanikio makubwa sana na kueleza kuwa anajivunia kwa kiasi kikubwa mafanikio hayo yaliofikiwa katika kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 na 2015-2020 pamoja na MKUZA II na MKUZA wa III.

Rais Dk. Shein ambaye pia, ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alieleza kuwa wananchi wataendelea kuiunga mkono CCM kutokana na juhudi zake za maendeleo ukuaji uchumi uliopatikana nchini.

Rais Dk. Shein aliwataka wananchi kuhakikisha huduma na miundombinu iliyofanywa na Serikali wanaitunza na kuitumia vizuri.

Alieleza umhimu wa kuongeza bidii ili uchumi uendelee kukua kwa kasi na nguvu zaidi ambapo alipoingia madarakani kasi ya ukuaji ilikuwa asilimia 4.3 na sasa ni asilimia 7.1, ukuaji huo umetoa mwelekeo vizuri wa kuweza Zanzibar kufikia nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020 huku akieleza dhamira yake kwa kipindi kilichobakia atafanya jitihada ya kuhakikisha kasi ya ukuaji uchumi inafikia asilimia 7.5 mnamo mwezi Juni mwakani.

Alieleza kuwa kwa upande wa mfumko wa bei umepungua kwani ulikuwa asilimia 6.1 alipoingia madarakani na hivi sasa umefikia  asilimia 3.9 jambo ambalo linaleta utulivu katika mwenendo wa biashara.

Alisema kuwa katika kipindi chake juhudi kubwa zimechukuliwa katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, ujenzi wa skuli za kisasa katika ngazi zote zikiwemo za Maandalizi,  Msingi na Sekondari.

Alifahamisha kwamba Skuli 13 za ghorofa zizmejengwa zikiweko 9 kutoka Mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na skuli tatu kutoka kwa Washirika wa maendeleo na moja aliyojengwa na mwananchi mzalendo Said Salim Bakhresa.

Alisema kuwa huduma za afya kwa upande wa Zanzibar zimeimarika kwa kiasi kikubwa ikilingalishwa na nchi nyengine za bara la Afrika na hata nje ya bara hilo.

Pia, alieleza jinsi Hospitali za Zanzibar zilivyopandishwa daraja sambamba na kuanzishwa  kwa utoaji wa huduma za usafishaji figo, saratani na nyengine za afya.

Alisema kuwa vituo vya afya vina kidhi mahitaji ya wananchi na mgonjwa haendi zaidi ya masafa ya kilomita 5 ya sehemu anayoishi kwa ajili ya kufuata huduma hizo.

Alifahamisha kwamba alipoingia madarakani kulikuwa vituo 135 na hivi sasa kuna vituo 160 Unguja na Pemba ambapo pia, sekta nyengine za maendeleo kama vile  kilimo, uvuvi nazo zimeimarika huku akieleza kuwa tayari meli mpya na kubwa ya uvuvi imeshawasili Zanzibar.

Kuhusua suala la uimarishajai wa sekta ya utalii alisema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta hii ambapo lengo lililobainishwa na Ilani la kupokea watalii 500,000 ifikapo mwaka 2020 tayari limeshafikiwa kabla ya wakati huo na kubainisha kwamba mwaka jana Zanzibar ilipokea watalii 52,0809.

Alibainisha kwamba hivi sasa kumekuwa na ongezeko la Mashirika ya kigeni kuleta wageni Zanzibar kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Urusi na Mataifa mengine ya Ulaya Mashariki na kueleza matumaini yake kwamba Zanzibar inaweza kupokea watalii 700,000 ifikapo mwaka 2020.

Alieleza kuwa kuwepo afya bure, elimu bure sambamba na kuwepo kwa miasingi ya utawala bora na haki za binaadamu ikiwemo uhuru wa kuabudu na kuwepo kwa uvumilivu wa dini hapa Zanzibar.

Hata hivyo, alieleza changamoto zilizopo ikiwemo suala zima la ajira ambapo tayari serikali imeweka miakati ikiwa ni pamoja na kuweka mifuko maalum ukiwemo ‘Mfuko wa kuwaewezesha kiuchumi wajasiriamali’ pamoja na ‘Mfuko wa  vijana’ ambapo kwa upande wa ‘Mfuko wa Vijana’ tayari Bilioni 46 zimetengwa.

Alieleza imani yake kwa wananchi kuwa wataendelea kuichagua CCM, na ameridhika kwamba Serikali anayoiongoza inafanya vizuri katika kuwatumikia wananchi ambapo na wananchi wenyewe wameridhika na uongozi wa Serikali yao ya Zanzibar.

Alieleza kuwa changamoto zipo na fedha hazitoshi lakini juhudi za makusudi zinaendelea kuchukuliwa na Serikali kwani hata hivyo, uwezo haujafikiwa asilimia 100 na kueleza kasi ya Mapinduzi ya kuwaweka wananchi katika mazingira bora ipo kwani miji 20 itajengwa sambamba na ujenzi unaondelea wa miradi kadhaa.

Rais Dk. Shein aliendelea kusisitiza kuwa amani na utulivu ndio suala muhimu katika maendeleo ya Zanzibar hatua ambayo imemfanya abuni mradi wa ‘Zanzibar Salama’ ili usalama uimarike sambamba na kuimarika kwa sekta ya utalii na  mazingira yake.

Alifahamisha kwamba hivi sasa utegemezi wa Bajeti ya Serikali umepungua kutoka asilimia 30.2 mwaka 2010 hadi asilimai 6 hivi sasa hali ambayo imechangiwa na juhudi kubwa zilizochukuliwa katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato.

Alisema kwamba misaada inayopatikana kutoka kwa wahisani  inatumika zaidi kwa miradi ya maendeleo.

Alisema kuwa Serikali inakusanya kwa mwezi TZS Bilioni 67 kwa mwezi ambapo mwaka 2010 Bilioni 13.5 na kuweza kuvuka lengo la Ilani ya CCM hatua ambayo imepelekea kununua vifaa kadha vikiwemo vya barabara, vifaa vya uchunguzi wa afya, dawa za kila aina na kupelekea kuwepo kwa afya bure na elimu bure.

Kwa upande wa suala zima la uzalilishaji wa wanawake na watoto, Rais Dk. Shein alisema kuwa Serikali inapiga vita na imeweka sheria kali katika kupambana na vitendo hivyo sambamba na dawa za kulevya, rushwa na maadili ya viongozi.  

Pia, Rais Dk. Shein aliendelea kusisitiza kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utadumisha na yeye na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Johm Pombe Magufuli watausimamia vyema.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.