Habari za Punde

EMANUEL GEKA WA KIDAMALI FC KINARA WA MAGOLI KABLA YA HATUA YA NANE BORA YA ASAS SUPER LEAGUE KUANZA

Wachezaji wa timu ya Kidamali inayoshiriki ligi ya mkoa wa Iringa maarufu kama ASAS SUPER LEAGUE  ambapo mchezaji wa timu hii Emanuel Geka anaongoza kwa ufungaji wa magoli hukupia timu ya kidamali ikiwa imefuzu hatua ya nane bora ya ASAS SUPER LEAGUE 
Wachezaji wa timu ya Kidamali inayoshiriki ligi ya mkoa wa Iringa maarufu kama ASAS SUPER LEAGUE  ambapo mchezaji wa timu hii Riziki Kelvin anaongoza kwa ufungaji wa magoli huku pia timu ya Isiman ikiwa imefuzu hatua ya nane bora ya ASAS SUPER LEAGUE 

Na.Fredy Mgunda. Iringa. 
WACHEZAJI nane kutoka timu za Mafinga Academy,Kidamali fc,Kalinga Fc,Isimani Fc, Mapanda Fc na Irole fc wanafukuzia tuzo ya mfungaji bora wa mashindano ya kugombea kombe la bingwa wa mkoa yanajulikana kwa jina la Asas Super League 2019 (ASL 2019).

Wachezaji hao vinara Emanuel Geka wa Kidamali anamagoli 8, Luka Duma (Irole fc) na Riziki Kelvin wa Isimani Fc wana magoli 7 kila mmoja Baraka Athumani kutoka Mafinga Academy na Vicent Madembo (Mapanda Fc) kila mmoja wana goli 5, Kelvin Msafiri (Kalinga Fc),Conrodgers (Irole Fc)na Mohamed Rashid (Isimani fc) wameonyesha uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu ambapo hadi sasa kila mmoja amefanikiwa kufunga magoli 4 katika michezo waliyocheza.

 Licha ya ushindani mkali katika mashindano hayo katika ufungaji mchezaji wa Kidamali fc Emanuel Geka anakimbizwa kwa karibu na mchezaji Riziki Kelvin wa Ismani ambaye anamagoli saba na alikuwa mfungaji bora msimu uliopita.

Mchezaji wa Kidamali fc Emanuel Geka amefunga magoli mengi akiwa katika uwanja wa kidamali tofauti na akiwa anacheza nje ya uwanja wao wa nyumbani hivyo amekuwa mmoja ya wachezaji ambao wanautumia vizuri uwanja wa nyumbani kufumania nyavu za wapinzani.

Katika mashindano hayo hadi sasa timu ya soka ya Irole Fc ndio kinara wa magoli mengi kwa kuwa na magoli 18 katika michezo 7 iliyocheza ikifatiwa na timu ya soka ya Isiman Fc yenye mabao 17 huku Kidamali Fc wakiwa na mabao 13 na hizi timuzote zinatoka katika kundi B na zimefuzu hatua ya nane bora ya Asas Super League.

 Timu za Acosato ndio timu iliyoruhusu magoli mengi kwenye michezo yao kwa kufungwa goli 15 huku ikifuatiwa na timu ya African wonders ambao wamefungwa magoli 14 huku zikifuatiwa na Magulilwa na mapanda fc ambazo zote zimefungwa magoli 12 kila. 

Aidha ligi hiyo hadi kufikia sasa jumla ya magoli 170 yamefungwa na timu zote zinazoshiriki ligi ya Asas Super League msimu wa 2019/2020

Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya maziwa ya Asas bingwa atapata kombe na sh. 2,000,000,jezi seti moja,mipira mitatu na cheti, na nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa wa mikoa.

Mshindi wa Pili shilingi 1,000,000, Mipira 2, Jezi Seti 1, Cheti cha Ushiriki huku Mshindi wa Tatu - Tsh 500,000/=, Jezi Seti 1, Cheti cha Ushiriki na zawadi nyingine ni kwa  wanahabari wameyatangaza vyema mashindano hayo kama ifuatavyo Mwandishi bora blog, Mwandishi bora wa luninga , Mwandishi bora Redio kipindi cha michezo na Mwandishi bora gazeti watapata sh. 50,000 kila mmoja.

Lakini pia kutakuwa na zawadi kwa kipa bora, mchezaji bora wa mashindano, mwamuzi bora,mfungaji bora , timu yenye nidhamu itaondoka na zawadi pia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.