Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Mihayo Juma Nhunga akikabidhi visaidizi kwa wazee wa watoto wenye mahitaji maalum katika hafla iliyofanyika migombani katika ofisi ya idara ya watu wenye ulemavu Zanzibar.
Na Ali Issa- Maelezo Zanzibar 20/11/2019.w
Naibu Waziri Wanchi Ofisi ya Makamu wa Pili Wa Rais Mihayo Juma Nhnunga amesema Visaidizi vilivyo tolewa kwa watoto wenye ulemavu ndio dhamira ya Serikali kuona kuwa walemavu wanasaidiwa ili kuwawezesha katika shughuli zao za kimaisha likiwemo suala zima la elimu.
Ameyasema hayo leo huko migombani zanzibar wakati akikabidhi vifaa hivyo kwa watoto hao katika hafla maalumu iliofanyika hapo.
Amesema Serikali imepeleka Madaraka mikowani ili kuona suala la kupatiwa huduma wananchi liwe jepesi na ukaribu.
Amesema vifaa waliopewa watoto hao nimuafaka kwani vitawarahisishia mambo yao.
"Sheria za Manispaa zinaeleza kuwa kupewa misaada wananchi kwa kuwasaidia ni moja ya jukumu lao"alisema Naibu Waziri.
Aidha alimesema watoto wenye ulemavu hupata tabu wakati wakifuatilia masomo yao katika masafa marefu jambo ambalo huwalazimu wazazi kuwabeba na kuwafikisha sehemu husika .
Aidha alisema utowaji wa visaidizi hivyo vitawafanyia wepesi wazazi wa watoto kwa kuwafikisha skuli kwa wakati na kuweza kufikia malengo waliojiwekea .
Naibu huyo aliwataka wazazi na walezi kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu na vinapo haribika kufanyiwa matengenezo.
Nae Afisa wa Halmashauri za Wilaya ya Magharibi "A" Yumna Ali Mwinjuma alisema msaada huo utakuwa endelevu kwa watoto wengine wenye mahitaji maalum.
akizungumza kwa niamba ya wazazi wenzake Juma Suleiman alisema kuwa visaidizi hivyo vimekuja wakati muafaka na watavitumia kwa dhamira iliokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuwapelekea skuli watoto wao wanaotoka masafa ya mbali.
“Shukurani kubwa kwetu kwa kupata wepesi kwani tulizowea kuwabeba watoto kuwapeleka sehemu tofauti za elimu na shughuli za kijamii “alisema Mzee huyo.
Visaidizi hivyo vimetolewa kwenye wilaya ya magharibi A na B kwa lengo la kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum kwa kukuza kiwango cha elimu nchini.
No comments:
Post a Comment