Habari za Punde

Kamati Yaridhishwa Hatua ya Mradi wa Ujenzi wa Makakama ya Kisasa Tunguu Zanzibar.

Mhandisi Ndg.Mussa Ali Hamad akitowa maelezo ya Ujenzi wa jengo la kisasa la Mahakamu Kuu Tunguu Wilaya ya Kati Unguja wakati wa ziara ya Kamati ya Sheria, Utawala bora na Idara maalumu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ilipotembelea Mradi huo kujionea maendeleo yake na hatua iliofikia ujenzi huo.
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria akitowa maelezo kwa Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar.Mhe.Khamis Juma Mwalim hiyo wakati wa ziara na Wajumbe wa Kamati ya Sheria, Utawala bora na Idara maalumu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipofika kutembelea Mradi huo wa Ujenzi wa jengo la Kisasa la Mahakama Kuu Zanzibar linalojengwa katika eneo la Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.Na Raya Hamad WKS24/1/2020
Kamati ya Sheria, Utawala bora na Idara maalumu ya Baraza la Wawakilishi imeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Mahakama Kuu Tunguu Zanzibar Mkoa wa Kusini Unguja Wilaya ya Kati.

Hayo yameelezwa na Makamo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Zulfa Mmaka Omar ambae wakati walipofanya ziara kuangalia ujenzi unaoendelea wa Mahakama Kuu Zanzibar katika eneo la Tunguu na baadhi ya Mahakama ikiwemo Mkokotoni na Mahonda pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji robo ya pili ya Oktoba – Disemba 2019 ya Wizara ya Katiba na Sheria.

Mhe.Zulfa amesema hatua iliyofikiwa ni nzuri hivyo ameitaka Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha wanasimamia ipasavyo kuona taasisi zote zinazohusika zinashirikiana katika kurahisisha upatikanaji wa rasilimali zinazohitajika katika ujenzi huo na kuweza kumalizika  kwa wakati uliopangwa.

Amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejipanga kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo na kukamilisha vipaumbele vya Serikali ambapo kati yake ni kukamilika kwa Ujenzi wa Mahakama Kuu Zanzibar ya kisasa katika eneo la Tunguu Wilaya ya Kati Unguja “macho ya Kamati hii ya Serikali na wananchi hivi sasa yanaangalia ujenzi wa Mahakama nasisitiza changamoto zilizopo zitatuliwe ili ujenzi ukamilike kwa wakati”

Aidha ameitaka Wizara ya Katiba na Sheria kuendelea kuboresha majengo ya mahakama za mikoa na wilaya Unguja na Pemba kwa kuyafanyia ukarabati ili majengo hayo yaweze kuwa na hadhi za mahakama.

Nae Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe.Khamis Juma Mwalim amesema changamoto zilizojitokeza hasa ya mchanga tayari zimeshapatiwa ufumbuzi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Maliasili zisizorejesheka na kuahidi kuendelea kutatua changamoto zitakazojitokeza ili azma ya Serikali iweze kufikiwa ili jengo hilo liweze kukamilika kwa wakati uliopangwa.

Mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar Mhe. Mohamed Ali Mohamed amempongeza Rais wa Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na Serikali kwa ujumla kwa kujenga na kufungua majengo mapya ikiwemo kufanyika kwa matengenezo makubwa ya majengo mbali mbali ya mahakama Unguja na Pemba na kuahidi kuyaenzi na kuendeleza ukarabati wa majengo yaliyobaki.

“Tunakusudia kuzikarabati upya Mahakama zetu zote na kurudisha haiba na uasilia hatutaondosha au kubadilisha bali tunazingatia vigezo na umuhimu wake nzima jengo yetu uimara na utekelezaji mzuri wa majukumu ya kazi kwa watendaji wetu ”alisisitiza Mrajis wa Mahakama Kuu
Zanzibar Mhandisi wa Mahakama Kuu Tunguu Ndg.Mussa Ali Hamad ameahidi jengo hilo kumalizika kwa wakati kwani changamoto kubwa zilizokua zikizorotesha ujenzi huo tayari zimeshatatuliwa.

Wakitoa michango yao wakati wa majumuisho baadhi ya wanakamati Kupitia Wizara wameomba kuwepo kwa mashirikiano kati ya waendesha mashtaka wapelelezi na Polisi ili waende sambamba na utowaji wa haki

Kwa upande mwengine wameitaka Ofisi ya Mufti kuandaa muongozo wenye kufuata utaratibu maalum wa ufundishaji kwa wanafunzi wa madrasa zakur-ani badala ya utaratibu uliopo sasa kila mwalima maUstadh kufundisha vile wanavohisi inafaa

Kamati imehimiza kuungana pamoja kwa taasisi za Serikali hasa zile ambazo zitakuwa zinategemeana mahitaji ili kurahisisha upatikanaji wa mahitaji ya lazima katika miradi ya maendeleo jambo ambalo litawezesha kukamilika kwa wakati kwa miradi iliyopangwa
Ujenzi wa Mahakama ya Tunguu umeanza rasmi tarehe 21 Octoba 2019 na unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na jengo hilo litakuwa la ghorofa nne

‘’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’
KamatiyaSheria, Utawala bora naIdaramaalumuyaBaraza la WawakilishiimeridhishwanahatuailiyofikiwayaujenziwaMahakamaKuuTunguu .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.