Habari za Punde

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC ) Yatoa Mafunzo Kwa Wakuu wa Vituo Uwandikishaji Wapika Kura Kisiwani Pemba.

 
AFISA Uchaguzi Wilaya ya Chake Chake Hafidh Ali Mohamed (Hafidh shoka), akimsikiliza mmoja ya washiriki wa mafunzo ya wakuu wa vituo, makarani wa uwandikishaji wa wapiga kura wapya kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) mkutano uliofanyika ukumbi wa skuli ya Madungu Sekondari.
MKUU wa Kurugenzi ya IT kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mwanakombo Machano Abuu, akiwaonyesha kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi  kwa wakuu wa vituo, makarani wa uwandikishaji wa wapiga kura wapya,  kitakachotambuliwa na Tume hiyo wakati wa uwandikishaji wapiga kura wapya
AFISA IT kutoka tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)Yussuf Mohamed Ali, akionyesha kwa vitendo jinsi ya kuskani kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, kwa wapiga kura wapya baada ya kumaliza kuingiziwa taarifa zake katika mashine ya uwandikishaji
BAADHI ya wakuu wa vituo na makarani wa uwandikishaji wa wapiga kura wapya, wakifuatilia kwa makini mashine ya VRD itakayotumika kuingizia taarifa za mpiga kura na uhakiki wake pia, wakati wa zoezi la uwandikishaji wapiga kura wapya utakapoanza hivi karibuni (PICHA NA ABDI SULEIMAN)

1 comment:

  1. shukran sana mablogger kwa kutuwekea taarifa kingajani..mungu azidi kuwaongezea maarifa

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.