Habari za Punde

Uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi wa Nyumba za Kwahani Jijini Zanzibar.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa, akitowa maelezo ya Ujenzi wa Mji Mpya wa Kwahani Jijini Zanzibar, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi huo unaofanyika katika eneo la kwahani


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kabla ya Mapinduzi ya 1964, Wazalendo wa Zanzibar walibaguliwa kwa makaazi kutokana na uwezo duni walionao.

Dk. Shein amesema hayo katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la msingi la ujenzi wa Mji mpya wa Zanzibar eneo la Kwahani, ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema wengi wa wananchi ikiwemo wafanyakazi waliishi katika maeneo ya 0ng’ambo kwenye makazi ya nyumba duni, huku wale wenye uwezo wakiishi katika maeneo ya mji Mkongwe na maeneo mengine ya kati ya mji.

Alisema katika uchaguzi wa mwisho wa mwaka 1963, Chama cha ASP kupitia Ilani yake ya uchaguzi kilitowa ahadi ya kuwapatia makazi bora wananchi wote, hatua iliyofuatiwa na ujenzi wa nyumbaza Kikwajuni (jumba la miguu) mara baada ya Mapinduzi kupitia msaada wa Serikali ya Watu wa Ujerumani.

Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi chini ya Uongozi wa Marehemu Mzee Abeid Aman Karume, iliendeleza dhamira ya kujenga nyumba bora za kisasa hatua kwa hatua, kwa kujenga nyumba katika eneo la Kilimani na hatimae Michenzani.

Aidha, alisema Mapinduzi ya 1964 yameondowa tofauti ya makazi iliyokuwepo kati ya mji mkongwe na ng’ambo,  ambapo hivi sasa mji wote unaonekana kuwa mmoja.

Alisema Serikali inamipango madhubuti ya kuendeleza ujenzi wa nyumba za aina hiyo katika maeneo mbali mbali ya mji ili kuunganisha mazingira yafanane na majengo ya Michenzani.

Alisema ujenzi huo utaunganisha majengo ya Michenzani Mall eneo la packing pamoja na nyumba za Michenzani, hivyo kuleta mandhari nzuri ya mji wa Zanzibar.

Aliwahakikishia wananchi walioondoshwa kupisha ujenzi katika eneo hilo kuwa mara baada ya ujenzi kukamilika watarudi eneo hilo na kuendelea kuwa wananchi wa Kwahani.

Alisema dhamira ya Serikali ni kuijenga Kwahani mpya ili wananchi waweze kuishi katika makazi bora zaidi na kujiletea maendeleo.

Aidha, alisema mara baada ya Mapinduzi ya 1964, kuna nyumba kadhaa zilitaifishwa na kuwa mali ya Serikali,  na kubainisha kuwa Serikali kupitia uratibu wa shirika la nyumba inazifahamu nyumba zote hizo, hivyo akawataka watu kuondokana na ghilba ya kuhodhi nyumba hizo.

Alisema ujenzi huo pamoja na mambo kadhaa ya maendeleo yanayoendelea kufanyika hapa nchini ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa  CCM ya mwaka 2015-2020.

Akigusia suala la malipo ya fidia kwa ajili ya shughuli za maendeleo, ikiwemo maeneo ya ujenzi, Dk. Shein alisisitiza kwa kusema kuwa ardhi na mali ya Serikali, hivyo akabainisha umakini wa Serikali katika kuhakikisha wananchi wote wenye haki ya kulipwa fidia wanalipwa kutokana na mali zao na sio umiliki wa ardhi.

“Serikali inatowa haki ya kutumia ardhi lakini sio yako, ikitakiwa anahaki ya kumpa mtu mwengine………..”,alisema.

Nae, Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia alisema uendelezaji wa makazi bora kwa wananchi wa Zanzibar, ulitokana na ahadi iliyotolewa katika Ilani ya ASP ya mwaka 1963 yakuhakikisha wananchi wote wanaishi katika makazi bora.

AlisemahatuayaserikaliyaawamuyasabailiyochiniyauongoziwaRais Dk. Ali Mohamed Sheinyakujenganyumbahizoniutekelezajiwamipangoiliyoanzishwanaviongoziwaliotangulia, akitoamfanowaujenziwanyumbazamaendeleokatikamaeneombalimbaliUngujana Pemba.

Alisemaujenziwamjimpyawa Zanzibar eneo la KwahaniunaashiriadhamirayaSerikaliyaMapinduziya Zanzibar yakujengamijiyakisasakatikamaeneombalimbaliUngujana Pemba.

Aidha, alisemaIlaniyaUchaguziya CCM yamwaka 2015-2020 inafikiakikomomwakahuu,akabainishamatumainiyakeyakuwepomaendeeoendelevukatikamiakaijayokwakuzingatiaurithiwa CCM kutokavyamavya ASP na TANU.

BaloziRamiaaliushukuruUongoziwaShehiyayaKwahani, CCM MkoaMjiniMagharibipamojanaKamatiyaFedhayaBaraza la Wawakilishikwakufanyajuhudikubwakuwahamasihawananchiwaeneohilokukubaliwazo la Serikali  lakuanzishaujenzihuo.

Mapema, KatibuMkuuWizarayaFedhanaMipangoKhamisMussa, alisemaujenziwamjimpyawa Zanzibar eneo la KwahaniunatekelezwakupitiaKampuniyaEstim Construction Ltd kwagharamayashilingiBilioni 19.6, ambapoawamuya kwanza yaujenzihuoulioanzaOktoba 2, 2019 unatarajiwakukamilikaifikapoSeptemba 31, 2020.

Alisemaujenzihuoutakaohusisha‘Blocks’ tatuutakuwananyumba 70 zakuishinamaeneo 56 yabiashara,wakatiambapo Blocks mbilizinazofananakilamojaitakuwanamajengomawilipachayenyenyumba 14 kilamojapamojanamaeneoyabiasharanakufanyajumlayanyumba 28 zakuishi.

Alisema‘Block’ la tatulitakuwanajengomojalenyenyumba 14, ambapokilanyumbaitakuwanavyumbavitatuvyakuishi, jiko, choo, stoopamojanaukumbi.

Aidha,alisemakilajengolitakuwa la ghorofasita, sambambanamjihuokuwanabarabarazandani, matangimawiliyamajipamojanahudumazaumeme.

MussaalisemakuwamradihuoumezingatiautekelezajiwaMkakatiwaKukuzaUchuminaKupunguzaUmasikini MKUZA 111 pamojanaIlaniya CCM ya 2015-2020.

Alisemakufuatiaujenzihuonyumba52 zilizokuwawakiishiwananchizilivunjwahukunyingine10  zikiwakatikahatuayakuvunjwailikutoanafasizaidiyakuendelezaujenzihuo, wakatiambapoSerikalitayariimeshalipafedhakuwawezeshawamilikikukodisehemunyinginenakufidiausumbufuwakuhama.

Alielezakuwabaadayahatuazaujenzikukamilikawananchihaowatarudieneohilonakupatiwanyumbampyabilamalipoyaziada.

AliushukuruMfukowaHifadhiyaJamii Zanzibar (ZSSF) kwakukubalikuikopeshaSerikalishilingiBilioni 20 iliziwezekutumikakuambatananamahitajiyamradiyatavyojitokeza.

Aidha,aliwashukuruwananchiwaKwahanikwauzalendonakuwamstariwambelekushirikiananaSerikalikufanikishaujenziwamakaazimapya.

AbdiShamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 
 E-mail: abdya062@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.