Habari za Punde

Uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi na Salama Uroa

 Muonekano mzuri wa Kibango cha uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na Salama wa Bambi – Uroa uliofanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyewakilishwa na Waziri wake Mh. Mohamed Aboud Mohamed
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na Wananchi wa Uroa mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji Safi na Salama wa Kijiji hicho akimuwakilisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na Wananchi wa Uroia mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji Safi na Salama wa Kijiji hicho akimuwakilisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Umati wa Wananchi wa Uroa wakifuatilia Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi na Salama wa Kijiji chao ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia Miaka 56.
 Msanii wa Kikundi cha Utamaduni cha Max Band Bambuti akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi na Salama wa Bambi – Uroa hapo Skuli ya Maandalizi ya Mrembo Uroa Wilaya ya Kati.
Baadhi ya Wananchi, Vijana pamoja na Wanafunzi wa Skuli wakifuatilia burdani ya Ngoma kutoka kwa Utamaduni cha Max Band.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis, OMPR

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia Wananchi wote kwamba haitosita kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma za Maji safi na salama hadi lengo la kuwafiki Wananchi Huduma hiyo linatekelezwa ipasavyo.
Utekelezaji huo ni muendelezo wa dhamira za Waasisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 wenye azma ya kwenda sambama na malengo yaliyowekwa na Jumuiya za Kimataifa katika kukidhi mahitaji ya Maji kwa Binaadamu ambayo ni chachu ya Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa hakikisho hilo katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh. Mohamed Aboud Mohamed kwenye uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na Salama wa Bambi – Uroa katika shamra shamra za kusherehekea Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema upatikanaji wa huduma za Maji safi na Salama huleta faida kubwa karika Jamii hasa kwa Wanawake na Watoto kupata nafasi ya kujishughulisha na harakati za maendeleo na Elimu mambo yanayochangia kuiwezesha Jamii kujenga Afya Bora.
Balozi Seif alisema baadhi ya Vijiji Nchini vilivyopakana na Bahari kama Uroa Wananchi wake wamekuwa wakitumia Maji ya Chumvi ambayo sio mazuri Kiafya na kufikia uamuzi wa kuwaondoshea shida hiyo kwa uchimbaji wa Kisima hicho.
Aliwaomba Wananchi wa Uroa na Vijiji vitakavyotumia huduma hiyo ya Maji safi na salama kuchangia huduma hiyo ili kuiwezesha Mamlaka ya Mazi Zanzibar {ZAWA} kumudu kuyalinda, kuyasambaza na kuyafanya maji kuwa hidaya inayoendelea.
Akitoa Taarifa ya kitaalamu ya Mradi huo wa Maji safi na salama wa Bambi – Uroa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Nd. Ali Khalil Mirza alisema Uoa ni Vijiji vilivyoanza kupta huduma ya Maji safi na salama mara tuu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Nd. Mirza alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ililazimika kufanya juhudi ya kuchimba Kisima kwa ushirikiano na Serikali ya Ras Al - Khaimah baada ya Maji waliyokuwa wakitumia kuchanganyika na Maji ya Chumvi.
Alisema Mradi huo wa Maji safi na Salama kutoka Bambi hadi Uroa wenye urefu wa Kilomita Nne uliogharimu zaidi ya Shilingi Milioni Mia 349,000,000/- utakuwa na uwezo wa kuzalisha Lita Laki 960,000 wakati mahitaji halisi ni Lita Laki 800,000 kukiwa na bakaa ya Lita Laki 160,000.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, maji na Nishati amewaomba Wananchi watakaofadikika na Mradi huo kubeba dhima ya kutoa Taarifa kwa Wahandisi wa Mamlaka  ya Maji pale inayotokea hitilafu ya kiufundi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kusini kwa niaba ya wananchi wa Mkoa huo Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud alisema wananchi wa Mkoa wa kusini wamefarajika  kutokana na kukamilika kwa mradi wa maji kutoka Bambi kwenda Uroa kwani kufanya hivyo kumeweza kuondosha changamoto iliyodumu kwa kipindi cha kirefu katika kijiji chao.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Ayoub alieleza kuwa serikali ya Mkoa wa kusini itaendelea kutimiza wajibu wake kwa kuizingatia sheria Namba nane (8) ya tawala za mikoa ya mwaka 2014 sheria ambayo inasisitiza juu ya usimamizi mzuri wa miradi ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto za kijamii ikwemo upatikanaji wa maji safi na salama.
Mh. Ayoub alisema mradi huo wa Bambi Uroa utasaidia kufaidisha Wananchi wa Shehia ya Uroa iliyozunguukwa na Vijiji Vinne wakati Shehia Saba ndani ya Wilaya ya Kati bado zinaendelea kukumbwa na tatizo la ukosefu wa Maji Safi na salama.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Kusini Unguja alizitaja Shehia hizo kuwa ni pamoja na Uzi, Ng’ambwa, Kikungwi, Tunguu, Cheju, Binguni pamoja na Ndijani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.