Habari za Punde

Waziri Mkuu Majaliwa aweka Jiwe la Msingi Hotel ya Golden Tulip Airport Zanzibar

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Royal Group Of Companies Hassan Mohammed Raza katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Hotel ya Golden Tulip Airport Zanzibar uliofanyika Kisauni Mjini Unguja.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikunjuwa Kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Hotel ya Golden Tulip Airport Zanzibar hafla iliofanyika Kisauni Mjini Unguja.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya  uwekaji wa Jiwe la Msingi Hotel ya Golden Tulip Airport Zanzibar hafla iliofanyika Kisauni Mjini Unguja.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Na Mwashungi Tahir     Maelezo    
WAZIRI Mkuu wa Serikali ya  Jamhuri Muungano wa Tanzania Kassim Majaaliwa  Majaaliwa alisema Serikali imeweka  mazingira mazuri katika uwekezaji kwa lengo la kukuza sekta ya utalii na  kukuza kipato nchini.
Hayo aliyasema huko katika uwekaji wa jiwe la msingi  wa ujenzi wa Hotel ya Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar ulioko Kisauni ikiwa ni shamra shamra ya kusherehekea miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Alisema Serikali imefanya maboresho makubwa katika kuwekeza ili kuvutia   watalii  na waweze kufika kwa wingi  na  kuongeza pato la Uchumi Nchini.
Hivyo aliwashukuru Marais wote wa Jamhuri yaMuungano John Pombe Magufuli na Dkt Rais Ali Mohamed Shein  kwa kusimamia sekta ya utalii na kufanya  juhudi za kushajihisha  uwekezaji na kutoa fursa kwa vijana.
Aidha alisema ujenzi wa hoteli ya Golden Tulip unaenda sambamba na kukuza uwanja wa ndege kwani viwanja vingi vya ndege havina hoteli karibu hivyo kuweka hoteli hiyo hapo   kutaweza kuwarahishia wageni katika usafiri wa kupanda ndege kwa ukaribu.
Pia aliwataka wanaodhamiria kujitokeza katika kuweka  uwekezaji Nchini wanakaribishwa fursa zipo na watapewa mashirikiano ili waweze kufanikisha kwa kupewa maboresho zaidi.
Alisema  watalii wanaokuja Zanzibar hupendelea sana kukaa karibu na fukwe na kuwapatia huduma ya  malazi yaliyo karibu na uwanja wa ndege na pia kuwarahisishia masafa wanapotaka kuondoka kuwahi ndege kwa wakati alimpongeza muwekezaji kwa kufanya wazo sahihi  katika  ujenzi huo.
“Umefanya maamuzi sahihi katika ujenzi wa hoteli karibu na uwanja wa ndege kwani kutawarahisishia wageni kuwahi ndege kwa wkati wanapotaka kuondoka”, alisema Waziri huyo.
Vile vile alisema mradi huu wa ujenzi wa hoteli hiyo ni kielelezo cha kukuza kasi ya utalii katika visiwa hivi na kuwataka wawekezaji kuweka kipa umbele  mambo ya asili ili kiwe kivutio zaidi kwa watalii wanaofika hapo.
Pia alisisitiza ulinzi uimarishwe ili kuwaweka wageni katika hali ya usalama wanapoingia hadi wanapotoka na kutaka iwekwe CCTV kwa ajili ya kuimarisha usalama zaidi kama ulivyowekwa mji Mkongwe.
“Nawaomba muimarishe ulinzi ndani ya eneo hili ili usalama uweze kuimarika na wageni wawe katika hali ya usalama wao na mizigo yao kwa kuwawekea CCTV”, alitoa msisitizo Waziri Mkuu Majaaliwa.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa alisema Serikali inazidi kuimarisha uwekezaji mwaka hadi mwaka sambamba na kuongeza uchumi na kukuza pato kwa kuongezeka watalii nchini.
Pia alisema wawekezaji wanazidi kuja kuwekeza katika visiwa vyetu vya Unguja na Pemba kwa kuwa kuna utulivu na amani na haya ndio Matunda ya Mapinduzi kuishi kwa amani.
Nae Ofisa mtendaji Mkuu wa Royal Group of Campanies Hassan Mohamed Raza alisema Hotel ya Golden Tulip ina vigezo vyote ambavyo vitawavutia wageni na kutaweza kuingizia mapato Serikali.
Alisema hadi sasa kampuni ina wafanyakazi 400 na asilimia kubwa ni wazanzibar na ujenzi ulianza tarehe 8-2-2019 na unatarajiwa kumalizika mwezi wa Septemba 2020 ambapo mradi huowa Golden Tulip umegharimu zaidi ya billion 20 .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.